Askari wa usalama Barabarani, akimkunja kijana aliyejitambulisha kuwa ni mwanafu wa Chuo cha CBE, aliyekuwa akjaribu kujibishana na kumbishia Askari huyo, wakati alipokuwa akitaka kukatiza katika njia iliyokuwa imefungwa kwa muda eneo la Makao Makuu ya CCM Mkoa wa Dodoma ili kupisha viongozi wa kiserikali waliokuwa wakiingia katika ukumbi huo.
Kijana huyo alikuwa akibisha kuhusu kufungwa kwa njia hiyo na kutowaruhusu kupita kabla ya kuanza kuingia kwa misafara hiyo.
Mwanafunzi huyo baada ya kuwekwa chini ya ulinzi baadaye aliachiwa huru baada ya kuomba msamaha kwa askari huyo.
Picha Na Sufiani Mafoto
No comments:
Post a Comment