Monday, August 1, 2011

Breaking Nuzz... mmoja akutwa maiti, watatu wakutwa hoi hoteli ya southern sun jijin dar

Mwili wa mmoja wa watu walaiokutwa chumba Na. 425 hoteli ya Southern sun jijini Dar
ukitolewa nje ya hoteli kupelekwa garini.

ULEVI wa kupita kiasi unaaminika kumuua raia mmoja wa Zambia na wengine watatu akiwamo Mtanzania, kubaki hoi na mmoja kuzindukia Muhimbili wakiwa katika Hoteli ya Southern Sun jijini Dar es Salaam.

Watu hao wanne ambao wote ni wanaume walikutwa katika chumba namba 425 ghorofa ya nne, kinachodaiwa kukodishwa na raia wa Kiingereza.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ilala, Faustine Shilogile alithibitisha tukio hilo na kusema wanaendelea na uchunguzi.

Aliyezinduka Muhimbili ni Eliud Sikwabi ambaye ni Muingereza na kuwataja wenzake kuwa ni Ikbar Bahabur wa Zambia na Mtanzania aliyetajwa kwa jina moja la Omari.
Kamanda Shilogile alisema inaonekana kuwa watu hao walikunywa kupita kiasi. Taarifa zaidi zinasema kwamba watu walianza kunywa katika sherehe ya harusi ya mtoto wa Jaji Mark Bomani, Clement.
Mwili ukipakiwa katika gari la wagonjwa tayari kupelekwa hospitali.
Wapelelezi wakiwa kazini kukusanya vielelezo kwa ajili ya uchunguzi
Habari kwa Hisani ya Issa Michuzi

No comments: