Tuesday, August 30, 2011

Jeshi La Polisi Mkoani Dodoma Laua Watuhumiwa Wanne wa Ujambazi Baada Ya Mapambano Makali


Kamanda wa Polisi wa mkoa wa Dodoma, Zelothe Stephen akionyesha bunduki iliyotengenezwa kienyeji inayosadikiwa walikamatwa nayo watuhumiwa wanne wa ujambazi waliouawa mjini humo wiki iliyopita katika majibishano ya risasi na polisi nje kidogo ya mji wa Dodoma.
Kamanada wa Polisi wa mkoa wa Dodoma, Zelothe Stephen akionyesha gamba lisilopenywa risasi lililonusuru maisha ya polisi wake katika mapambanao na majambazi katika pori la Goma, barabara ya manyoni-Singida nje kidogo ya mji wa Dodoma, wiki iliyopita. katika tukio hilo watuhumiwa wanne wa ujambazi waliuawa na polisi
Wananchi wakijaribu kunyanyua ili kujua uzito wa gamba lisilopenya risasi ambalo lilinurusu maisha ya polisi yaliokuwa wakipambana na majambazi wa kurushiana risasi katika msitu wa Goama, nje kidogo ya mji wa Dodoma wiki iliyopita.
Wananchi watazama maiti za watuhumiwa wa ujambazi iliyowekwa katika chumba cha maiti hospitali ya mkoa wa Dodoma
wananchi wakipanga foleni kuingia chumba cha maiti cha hospitali ya mjini Dodoma kutambua maiti za watu wanne waliouawa na polisi katika majibishano ya risasi wakituhumiwa kwa ujambazi wa kuteka mabasi katika barabara kuu ya Manyoni-Singida.
Kamanda wa Polisi mkoa wa Dodoma Zelothe Stephen na Mkuu wa mkoa wa Dodoma Dk James Nsekela na Mganga Mkuu wa hospitali ya Dodoma, Dk. Godfrey Mtei wakitoka katika chumba cha maiti kwenye hospitali hiyo Picha zote na Emmanuel Ndege -Eneo la Tukio Dodoma


No comments: