Mkurugenzi wa Masoko wa Kampuni ya Bia Tanzania, David Minja akisaini mkataba mpya wa udhamini kwa vilabu vya Yanga na Simba utakaodumu kwa miaka mingine mitano katika hoteli ya Double Tree,jijini Dar.
Makamu Mwenyekiti wa Simba,Godfrey Nyange 'Kaburu'akisaini Mkataba huo.
Makamu Mwenyekiti wa Simba,Godfrey Nyange 'Kaburu'akipongezana na Mkurugenzi wa Masoko wa TBL,David Minja mara baada ya kusaini mkataba huo.
Kiongozi wa Simba,Kaburu (kushoto) na kiongozi wa Yanga,Nchinga (kulia) wakiwa na furaha baada ya kusaini mikataba yao mpya na TBL,Pili kulia ni Katibu Mkuu wa TFF,Angetile Osiah na Mkurugenzi wa Masoko wa TBL,David Minja.
Na Francis Dande
KAMPUNI ya Bia Tanzania (TBL) kupitia Bia yake ya Kilimanjalo
Premium Lager ambacho pia ndiyo mdhamini mkuu wa vilabu vya Simba na Yanga, leo imesaini mkataba mpya utakaodumu kwa miaka mingine mitano katika hoteli ya Double Tree.
Mwaka 2008 bia ya Kilimanjaro ilikuwa mdhamini rasmi wa kwanza kwa Simba na yanga ambazo ni timu kubwa mbili kongwe, zenye upinzani wa jadi na mashabiki wengi zaidi nchini. TBL ilisaini mkataba wa kwanza Mwaka 2008 Ambao ulidumu kwa miaka mitatu.
Akiongea jijini Dar es Salaam na waandishi wa habari katika Hoteli ya Double Tree, Mkurugenzi wa Masoko, David Minja alisema “Kupitia Kauli mbiu ya Kilimanjaro premium Lager TBL itakuwa inafikisha soka la Tanzania kwenye kilele cha mafanikio kwa kuwa tumemaliza awamu ya kwanza ya udhamini wetu uliodumu kwa miaka mitatu kwa amani tumeonelea ni vyema kuongeza muda wa udhamini wetu kwa miaka mingine mitano ambayo tunauhakika kuwa kupitia udhamini huu Klabu zote mbili zitaendelea kufanya vizuri katika mashindano mbali mbali ndani na nje” Udhamini umegusa maeneo yafuatayo
1. Mkataba huu utaanza rasmi kuanzia tarehe 01/08/ 2011 mpaka tarehe 31/ 07/2016
2. Fedha ya Mshahara kwa mwezi imeongezeka kutoka milioni 16 kwa mwezi mpaka milioni 25 kwa mwezi. Na ongezeko la asilimia 10 kila mwaka.
3. Tutatoa basi jipya kabisa la abiria 54 kwa klabu zote mbili (54Seater)
4. Tutatoa fedha kwa klabu zote mbili kwa ajili ya kuendesha Mkutano Mkuu wa mwaka ( Annual General meeting)
5. Tutatoa shilingi milioni ishirini (20milion) kwa kila klabu kwa ajili ya kuandaa Simba day na Yanga Day Kila mwaka
6.Vifaa vya mechi mazoezi vimeboreshwa kutoka milioni 30 mpaka millioni 35 kwa kila msimu wa ligi
7. Zawadi kwa mshindi wa kwanza na wa pili kwa ligi inakuwa sh milioni 25 kwa mshindi wa kwanza na milioni 15 kwa mshindi wa pili.
Aliongeza “Tunavishukuru vilabu vyote viwili kwa kukubali tena kushirikiana na Kilimanjaro Premium Lager kwa awamu nyingine tena..
Hii inaonyesha kuwa udhamini wa Kilimanjaro premium lager utaendelea kuwa chachu ya mafanikio haya kwa vilabu hivi na Tanzania kwa ujumla. Kilimanjaro Premium Lager inatangaza rasmi kuwa imeendeleza mkataba huu na vilabu hivi viwili tukiamini kuwa udhamini huu utasaidia kutoa matokeo mazuri zaidi kwa Msimu wote wa ligi kuu ya bara pamoja na mechi zote za kitaifa na kimataifa. Kama mkataba unavyoainisha, Kilimanjaro premium Lager imeboresha mkataba wake na inategemea kutumia zaidi ya Shilingi Bilioni Tano ( 5 billioni)
Bw Minja aliendelea kwa kuvitaka vilabu viheshimu vigezo na masharti yaliyoainishwa kwenye mkataba.
Akizungumzia udhamini huu wa TBL kwa timu kongwe za Simba na Yanga, Katibu Mkuu wa TFF Bw Angetile Hosea Alisema “Mchango wa TBL kwa soka la Tanzania ni mkubwa sana kwani huku ndiko wachezaji wa timu ya taifa wanakotokea. Udhamini huu umewahamasisha wachezaji wa vilabu vyote viwili vikongwe.
Sisi kama TFF tunatarajia udhamini huu utaendelea kuwa wa manufaa kwa vilabu hivi na taifa kwa ujumla.
No comments:
Post a Comment