| Mkurugenzi wa Mamlaka ya Usimamizi wa Nishati na Maji, Dr Haruna Masebu, akizungumza na waandishi wa habari leo mchana ofisini kwake jijini Dar es Salaam. Masebu alisema kuwa, wauzaji na wamiliki wa vituo vya mafuta watakaobainika kuuza mafuta kwa bei ya zamani au kugoma kuuza mafuta watafutiwa leseni zao za biashara sambamba na kulipa faini ya Tsh 3 Milioni kila siku kwa kipindi chote watakapobainika kuwa wamegoma ama kukaidi kushusha bei. Aliongeza kusema kuwa bei mpya za nishati ya Mafuta ni halali na mchakato wa kupunguza bei hizo umezingatia gharama za ununuzi, usafiriahaji na uuzaji., hivyo ana uhakika kuwa bei mpya haiwezi kuwasababishia hasara wauzaji wa nishati hiyo. |
No comments:
Post a Comment