Mwenyekiti wa Taasisi ya WAMA Mama Salma Kikwete akipokea hundi ya shilingi milioni tano (5m/-) kutoka kwa Mkurugenzi wa Masoko wa Benki Bank ya CRDB Bi Tully Mwambapa (kulia)kwa ajili ya kuchangia tamasha la wajasiriamali wanawake (MOWE) 2011 usiku wa kuamkia leo jijini Dar es Salaam, Zaidi ya shiligi 55 milioni zimechangwa.(55,368,500/-)
Mkurugenzi wa Shirika la Kazi Duniani nchini Alexio Musindo akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa uchangishaji wa fedha kwaajili ya Tamasha la wajasiriamali (MOWE) yaani Month of Women Enterprenuers
Mwenyekiti wa Taasisi wa WAMA pia Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akiongea na Wajasiriamali wakati wa hafla ya uzinduzi wa uchangishaji wa fedha kwaajili ya Tamasha la Wajasiriamali (MOWE) 2011 litalofanyika jijini Dar es Salaam, ambapo mwaka huu Taasisi ya WAMA ndio mratibu wa Tamasha hilo.Jumla ya zaidi milioni 55 zimechangwa katika hafla hiyo na kauli mbiu ya mwka huu ya MOWE ( MIAKA 50 WANAWAKE WAJASIRIAMALI TUNAWEZA-TUTUMIE FURSA),(kulia ni Mwenyekiti wa MOWE Tanzania Elihaika Mrema,na (kushoto) ni Mwakilishi wa Katibu Mkuu kutoka Wizara ya Viwanda na Biashara Consolata
Baadhi ya Wanawake wajasiriamali wakifuatilia hotuba ya mgeni rasmi Mwenyekiti wa Taasisi ya WAMA Mama Slama Kikwete (Aug 26,2011) katika hafla ya uzinduzi wa uchangishaji wa fedha kwaajili ya Tamasha la wajasiriamali (MOWE) jijini Dar es Salaam
Michango ikiendelea.
Picha zote na Mwanakombo Jumaa-MAELEZO
Picha zote na Mwanakombo Jumaa-MAELEZO
No comments:
Post a Comment