Wednesday, August 17, 2011

Meja Jenerali wastaafu wa JWTZ waagwa

Maafisa wa Jeshi la wananchi Tanzania na Jeshi la Kujenga Taifa wakisukuma gari maalum kwa ikiwa ni ishara ya kuwaaga Mameja Jenerali wastaafu wa Jeshi hilo mara baada ya gwaride rasmi la kuwaaga jana katika Kambi ya Abdallah Twalipo jijini Dar es salaam. Kulia ni Meja Jenerali (mstaafu) Yodan Mtaluma Koyi na Meja Jenerali(mstaafu) Salim Suleiman.
Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama,Jenerali Davis Mwamunyange (katikati) akiongea na waandishi wa habari jana katika kambi ya Abdallah Twalipo jijini Dar es salaam mara baada ya gwaride rasmi la kuwaaga Mameja Jenerali na Brigedia Jenerali waliostaafu.

Na Mpoki Ngoloke-Maelezo,Dar-Es-Salaam Mkuu wa majeshi ya ulinzi na jeshi la kujenga Taifa Jenerali Davis Mwamunyange, Jana aliwaongoza maafisa wa kijeshi katika gwaride la Tafrija ya kuwaaga Mameja jenerali na mabrigedia jenerali wastaafu yaliyofanyika katika kambi ya jeshi ya Abdalah Twalipo. Katika gwalide na tafrija hiyo maafisa waagwa wenye vyeo vya Meja Jenerali na Brigadia Generali walipokea salam ya Jenerali, kukagua gwaride ambapo lilipita mbele kwa heshima kwa mwendo wa pole na haraka. Maafisa hao ni Meja Generali Yodan Kohi na Meja Jenerali Salim Suleiman wengine ni Brigedia Jenerali Wilfred Kabunda, Brigedia Jenerali Albert Barati na Brigedia Jenerali Francis Mndolwa, wengine ni Brigedia Jenerali William kihiyo na Brigedia Jenerali Mabala Mashauri. Katika tafrija hiyo, Generali Mwamunyange amesisitiza utii na heshima kuigwa kutoka kwa wastaafu hao. ”tumewaaga kwa namna hii ndiyo maana tumewaaga kila mmoja kwa nafasi zao’’ alisema

Picha na Tiganya Vincent, MAELEZO- Dar es salaam 

No comments: