Thursday, August 11, 2011

MSIBA MWANZA, MWANDISHI WA HABARI AUAWA KINYAMA


TANZIA: Imenichukua muda kuamini, pengine hii ndiyo sababu ya kuchelewa kuwafahamisha kuwa Tasnia ya Habari Mwanza imepata pigo kubwa baada ya Mwandishi Richard Masatu ambaye pia alikuwa Mkurugenzi wa Gazeti la KASI MPYA kufariki Dunia akiwa anapatiwa Matibabu katika Hospitali ya Mkoa ya Sekou Toure.

Taarifa za awali zinaonyesha kuwa Marehemu amekufa kutokana na majeraha ya kushambuliwa na watu wasiojulikana. Kwa sasa mwili wake upo Hospitali ya Rufaa ya Bugando kwa Uchunguzi kutokana na kukutwa na majeraha ya kuchomwa na kitu chenye ncha kali, chini ya Kidevu, jicho la kulia ikiwa na kupigwa na kitu kizito usoni upande wa kushoto.

Ina lilah wa ina illah rajiun, Bwana alitoa bwana ametwaa jina lake liabudiwe.

Habari hii kwa hisani ya Frederick M. Katulanda.

1 comment:

Anonymous said...

Am not happy! May he RIP. Mara ya mwisho alikua anaandika kuhuisu nn?