Mkurugenzi Mkuu na Meneja Mwendeshaji wa Precision Air Alfonse Kiako,(katikati) Mkurugenzi wa Biashara Phil Mwakitawa (kulia) na Meneja Mauzo Tuntufye Mwambusi wakiwauwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Nyerere wakisubiri kuzinduliwa kwa safari ya kwanza ya Ndege ya kampuni hiyo kutoka Dar es Salaam kwenda Johannesburg Afrika kusini jana.
Mwenyekiti wa Bodi ya Kampuni ya Precision Air Michael Shirima (kushoto) akitoa maelezo kwa abiria waliokuwa wakisafiri kwenda Johannesburg wakati wa uzinduzi wa safari ya kwanza ndege ya kampuni hiyo kutoka Dar es Salaam kwenda Johannesburg Afrika kusini, hafla hiyo ilifanyika jana katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Nyerere Dar es Salaam.
Baadhi ya abiria wakisubiri kusafiri na Ndege nambari PW 700.Boeing 737-300 ya Shirika la ndege la Precision Air ambayo ilizindua safari yake jana kati ya Dar es Salaam kwenda Johannesburg Afrika Kusini, kwa promosheni ya Dola 57 ili kuwawezesha watu wengi kusafri na shirika hilo.



No comments:
Post a Comment