Raia wa Ujerumani, VEIXLAR MARLM (24), WEIXLER ROLAND (21) wamenusurika kuuawa baada ya kutekwa na watu waliojifanya waendesha biashara ya Taxi katika kituo cha Ubongo jijini Dar es salaam. Raia hao waliwasili Ubongo Bus kituo kikuu cha mabasi Ubungo, jana jioni wakitokea Mombasa wakielekea Zanzibar. Walikodi Taxi Bubu, namba T 983 BDV Toyota Mark II Baloon, ambayo waliiomba iwapeleke Ferry kwa safari ya kwenda Unguja, lakini wakashangaa kujikuta wanapelekwa mitaa ya Sinza Makaburini. Waliposhitukia mchezo mchafu, wakaanzisha vurugu iliyowafanya dereva wa TAX hiyo na msaidizi wake kukimbia na kulitelekeza gari lao, ambalo baada ya kufanyiwa upekuzi sakari wa doria walikuta karatasi ya mkataba wa kuuziana gari na vitu vinavyodaiwa kuwa ni dawa za kulevya. Haikuweza kujulikana mara moja vitu walivyoporwa raia hao wa kigeni ambao walikuwa hawataki kupigwa picha. Gari lililotelekezwa na majambazi haopamoja na wagen hao walipelekwa kituo cha polisi cha Mbatini Kijitonyama kwa uchunguzi zaidi. Aidha taarifa zilizopatikana eneo la tukio, zimedai kuwa gari hilo limesharipotiwa katika tukio lingine la ujambazi. (Chanzo, Global Publishersblog)
|
No comments:
Post a Comment