Saturday, August 13, 2011

TAMKO RASMI KUTOKA KWA RUGE MUTAHABA KUHUSU MBUNGE WA MBEYA MJINI-CHADEMA MHESHIMIWA JOSEPH MBILINYI(MR II)




Ruge Mutahaba



--



Leo
asubuhi mida flani kati ya saa tano na saa sita, Tanzania imeshuhudia
kitendo ambacho kwa mtazamo wangu na kwa jinsi ninavyo elewa na ninavyo
heshimu bunge tukufu la jamhuri ya muungano wa Tanzania….ni kitu
ambacho tukikifungia macho, basi tutakuwa tunaruhusu bunge hili
kutumukia kama sehemu ya watu kumalizia matatizo yao binafsi na watu au
kundi la watu….


Itafika mahali, mbunge wa Bunge letu akiwa na chuki zake binafsi tu
akaamua kutumia jukwaa alilopewa kumuanzishia kashfa yeyote ile kwa hata
muuza machungwa wa kibanda ambacho hakipendi kila siku, hadi mwisho wa
siku watu wakanza kuamini hizo kashfa na ghafla uongo ukaanza kufanana
na ukweli. Hayo unategemea yatafanywa na wahuni, watu wanafiki lakini
sio wabunge wetu.



Hapa nazungumzia kitendo cha mbunge wa mbeya mjini bwana j mbilinyi
kuchukua nafasi yake kama mbunge ndani ya bunge hili kuikashifu kampuni
ya clouds media, asasi isiyo ya kiserekali ya tht na kwa kiwango
kikubwa na katika hali ya kusikitisha, kunikshfu mimi binafsi….



Naomba ieleweke kwamba mimi kama mimi, sina tatizo lolote na kashfa
ambazo bwana mbilinyi amekuwa akizilimbikiza kwangu kwa kuwa kwanza
licha ya ubunge wake, sugu ni mdogo wangu na daima kaka huwa ana busara
pale ambapo inonekana mdogo wake anatoka nje ya mstari….cha pili, style
yake ya kutolea kashfa zake kwa kutumia matusi kwenye facebook,
kurekodi cd zenye matusi, kutishana kwenye blogs sio style yangu.
Angeweza kuweka hoja mezani, kwa sababu wote ni Watanzania ningezijibu
ila kwa style hiyo nikijibu na mimi narudi kwenye level hiyo ya Kihuni.


….sababu ya tatu ni kwamba sidhani kwamba sugu anatoa kashfa hizo kwa
kuwa ana chuki binafsi na mimi bali ni mtu ambae ana ndoto flani ambazo
kwa njia moja au nyingine ana hisi daraja rahisi la ndoto hizo ni
kupitia kunichafua mimi…na kwa hilo, nimemuomba Mungu muda mrefu anipe
ustahimilivu wa kupokea matusi na kashfa zake zote ili mradi sehemu
kubwa ya wananchi kwa namna sahihi wanafahamu au watafahamishwa ukweli
na vyombo husika. Mi sitazizungumzia hoja alizozitoa kwa undani
kwasababu hakuwa anazielekeza kwangu bali kwa Waziri mwenye dhamana, Mh
Emmanuel John Nchimbi ambaye kutokana na majibu yake nitatoa ufafanuzi
wa hoja ambazo zinahitaji ufafanuzi zaidi.



Kinacho niuma zaidi ni pale kijana wa kitanzania, sugu, anatumia fursa
aliopewa na vijana wa kitanzania wa mbeya, kuwa kashfu vijana wa
kitanzania ambao wanashiriki kwa hiari kwa njia moja au nyingine katika
tamasha la fiesta kama wasanii au waajiriwa wa kazi mbali mbali
zitokanazo na tamasha hili ambalo liko katika mwaka wake wa kumi.
Tamasha hili liko chini ya kampuni binafsi kwa jina primitime promotion,
kampuni ambayo iko chini ya kampuni mama clouds media group, ambayo
pia humu ndani zipo redio station 3, clouds fm, choice fm, coconut fm
na cloud tv. Kwa kuwa ni kampuni binafsi, hapa sio sehemu ya kutangaza
utaratibu wake wa kufanya kazi lakini kw akuwa ni kampuni iliosajiliwa
kihalali hapa nchini, basi mtanzania yeyotea anaeniskiliza sasa hivi
ajue kwamba inaendeshwa chini ya sheria za nchi hii na kama ingekuwa
inafanya chochote kinyume na sheria za nchi hii basi vyombo husika
vingekuwa vimechukua mkondo wake..


Bwana sugu kwa jazba na hasira ambazo kwa mtazamaji wa kawaida wa
matukio ya bungeni, ni kitu ndara sana kuona muheshimiwa akikifanya,
alidiriki kuishambulia asasi isio ya kiserekali ambayo mimi ni
muanzilishi, Tanzania house of talent. Naomba bwana sugu aeleze
watanzania ni nini walimkosea vijana hawa wa kitanzania ambao wanajaribu
kujikwamua kutoka maisha ya dhiki kupita vipaji vyao ndani ya nyumba
hii ya vipaji. Kwa kuwa mimi sio msemaji wala manager wa tht, nasubiri
tht waje wamjibu sugu kuhusiana na tuhuma zake ingawa imenishangaza
inakuwaje mbunge anashindwa kufanya utafiti kidogo tu wa kugundua kuwa
THT ina nyumba mbili inazotumia na zote zinalipiwa kodi. Kwa miaka
mitano sasa sijapata hiyo bahati aise…..kodi, umeme, maji wote unalipwa
na THT yenyewe.



Sasa hebu jiulize, mbunge anachukua maneno barabarani na bila hata
kutafiti anayapeleka bungeni…hiyo ndo hali inayonitia wasiwasi kidogo.
Sio mixtapes, interviews , blogs na hata face book…joseph mbilinyi
amekuwa akitutukana wazi wazi mimi pamoja na wote hapa clouds fm….tht na
hata wasanii wengine anaowaita masnitch sababu wamefanya Fiesta kwa
ujumla…tumekaa kimya muda wote huo kwa kuwa tulikuwa tunampuuzia lakini
kitendo cha mtu huyu kutumia nafasi yake bungeni kuwapotosha watanzania
walio wengi kuhusiana na swala la mastering studio, pango la THT,
tamasha la fiesta na kadhalika ni jambo ambalo tukilifumbia macho
mwishoe atatukania wazazi wetu..


Pamoja na kwamba umekuwa unailalamilia TFU kwa ujumla, naomba
nikupongeze kwa walau kutumia baadhi ya vipengele ambavyo TFU
waliambatanisha katika maombi kumi na mmoja walio wasilisha kwa raisi.
Maombi hayo ni pamoja naTRA kuhusika katika kutoa sticker ambazo
zitatambulisha kazi halali za sanaa Tanzania, kuundwa kwa mamlaka ambayo
itasimamia haki za wasanii na sio COSOTA. Kwa kuwasilisha hoja hizo,
ulionyesha chembe chembe ya kile ambacho natumai ndicho
kilichowapelelkea wakazi wa mbeya mjini kukupa hsehima ya kukuchagua
kama mbunge wao.


Kwa kumaliza, nasema, siku zote naamini binadamu hatuna haters ila tuna a bunch of confused admirers.




RUGE MUTAHABA



No comments: