Tuesday, August 16, 2011

VODACOM FOUNDATION YAFUTURISHA JIJINI MWANZA



Viongozi na waumini wa dini ya Kiislamu wakihudumiwa futari katika hafla hiyo ya kufuturisha watoto yatima na wanafunzi wa madarsa jijini Mwanza. Wa pili kushoto ni Mkuu wa Vodacom Foundation Yessaya Mwakifulefule.

Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Abbas Kandoro (wa pili kuli) akikabidhi sadaka ya futari kwa wanafunzi wa madrasatul Munawar Lumara ya jijini Mwanza iliyotolewa na mfuko wa kusaidia jamii wa Vodacom Foundation ikiwa ni sehemu ya kampeni ya 'Vodacom Share and Care'. .


Vijana wa kiislamu kutoka Madrasatul Munawara Lumara ya Jijini Mwanza wakiburudisha katika hafla ya kufuturisha watoto yatima na wanafunzi wa madrasa jijini Mwanza iliyoandaliwa na Vodacom Foundation.

Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Abbas Kandoro (wa pili kulia) akikabidhi sadaka ya sabuni kwa wanafunzi wa madrasatul Munawar Lumara ya jijini Mwanza iliyotolewa na mfuko huo .
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Abbas Kandoro (wa pili kulia) akikabidhi moja ya vyerehani vitano kwa akina mama wa kikundi cha Jukato cha jijini Mwanza, vilivyotolewa na mfuko wa kampuni ya Vodacom wa kusaidia jamii, wa Vodacom Foundation ikiwa ni sehemu ya kampeni ya 'Vodacom Share and Care' inayoendeshwa kila mwaka wakati wa mfungo wa Ramadhan kusaidia yatima na wajane.Kulia ni Mkuu wa mfuko huo Yessaya Mwakifulefule. Hafla hiyo ilifanyika muda mfupi kabla ya Vodacom kufuturisha mamia ya watoto yatima,wajane na wanafunzi wa madrasa za jijini humo wishoni mwa wiki.


No comments: