Friday, August 26, 2011

Warsha kuhusu Mpango Kazi wa Umoja wa Mataifa Tanzania - UNDAP yafanyika jijini dar leo.

Pichani kulia ni Muwakilishi wa Shirika la kazi-Tanzania (ILO),Bwa.Antony Rutabandibwa akifafanua zaidi kuhusiana na kitabu kinachoelezea kwa ufupi athari kubwa kwa Watoto zitokanazo na kazi za ndani, kwenye warsha ilioandaliwa na Ofisi ya Mratibu Mkazi na Mwakilishi wa Umoja wa Mataifa Tanzania ikiwakilisha mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini Tanzania,na kuwaalika waandishi wa habari na pia kuwafahamisha juu ya vipaumbele kumi vya programu hii na utekelezaji wake,Warsha hiyo imefanyika leo asubuhi katika hoteli ya Movenpick, jijini Dar es Salaam.Pichani kushoto ni muwakilishi wa UNESCO.
Ofisa Mawasiliano UNDAP Tanzania Usiah Nkhoma Ledama akifafanua mbele ya waandishi wa habari kuhusiana na Umoja wa Mataifa Tanzania kuanza kutekeleza program mpya ya miaka minne inayojulikana kama Mpango wa Msaada wa Maendeleo wa Umoja wa Mataifa - (UNDAP) 2011-2015, inayolenga kusaidia maendeleo ya Tanzania kiuchumi, kijamii na kisiasa.
Warsha hiyo iliandaliwa na Ofisi ya Mratibu Mkazi na Mwakilishi wa Umoja wa Mataifa Tanzania ikiwakilisha mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini Tanzania,kwa Waandishi wa Habari ili kuwafahamisha juu ya vipaumbele kumi vya programu hiyo na utekelezaji wake. (ukitaka kujua viapaumbele hivyo,bofya clip ya video hapo juu).
Pichani kati ni Muwakilishi kutoka UN-Tanzania,ambae alikuwa akitoa ufafanuzi mbele ya Waandishi wa habari kuhusiana na namna gani Umoja wa Mataifa Tanzania utaweza kuisaida Tanzania katika moja ya vipaumbele vyake kumi vya programu hiyo (Utawala Bora) na utekelezaji wake,shoto kwake ni Dada Nora Mpendaeli kutoka UN-Tanzania.
Pichani kulia ni Mratibu wa Shirika la Chakula Duniani-Tanzania (FAO),Dr.Vedasto Rutacholozibwa akitoa ufafanuzi mbele ya Waandishi wa habari kuhusiana na namna gani Umoja wa Mataifa Tanzania utaweza kuisaida Tanzania katika moja ya vipaumbele vyake kumi vya programu hiyo (ukuaji wa uchumi) na utekelezaji wake.
Mtaalamu wa masuala mbalimbali ya Watoto kutoka UNICEF-Tanzania,Dada Mona Aika akifafanua jambo kwa mmoja wa Waandishi wa habari aliyehudhuria warsha hiyo iliyofanyika kwenye hoteli ya Movernpick jijini Dar leo.
Afisa Habari kutoka Ofisi ya Mratibu Mkazi na Mwakilishi wa Umoja wa Mataifa Tanzania (UN-Tanzania),Hoyce Temu akiwakaribisha wanahabari na wageni waalikwa katika Hoteli ya Moevenpick jijini Dar leo,kwenye Warsha iliyohusu Umoja wa Mataifa Tanzania kuanza kutekeleza program mpya ya miaka minne inayojulikana kama Mpango wa Msaada wa Maendeleo wa Umoja wa Mataifa - (UNDAP) 2011-2015, inayolenga kusaidia maendeleo ya Tanzania kiuchumi, kijamii na kisiasa.
Baadhi ya Waandishi wa habari pamoja na wageni waalikwa mbalimbali waliohudhuria warsha hiyo
Pichani ni Waratibu wa warsha hiyo iliyofana kwa kiasi kikubwa.

No comments: