Saturday, September 10, 2011

FFU Ughaibuni ! Kupigwa kwata Bremen City,Ijumaa 16.09.2011

Kile kikosi kazi cha FFU Ughaibuni aka Ngoma Africa band,kinatarajiwa kutua mjini Bremen,ujerumani siku ya ijumaa 16.09.2011 kwa kazi moja tu..ya kuwadatisha akili washabiki na mdundo wa muziki "made in Uswahilini" katika onesho kubwa la aina yake "AFRIKA MESSE" ambalo limeandaliwa na shirika lisilo la kiserekali GIZ International.

Ngoma Africa band inayoongozwa na kamanda ras Makunja,ina utajili wa wanamuziki wenye vipaji wakiwemo akina Diva Bedi Beraca,Said Vuai,Christian Bakotessa aka Chris-B na wengineo.kikosi kazi hiko chenye tabia za kuwatia kiwewe washabiki wake kila wanapotumbuiza,kimejikuta kina kazi ya ziada ya kuwapa washabiki " Extra Ordinary Bongo dansi" made in Uswahilini.

Tafadhali wasikilize FFU at www.ngoma-africa.com

No comments: