Sunday, September 25, 2011

Hongera Cathbert kajuna na da' Easter Ulaya walio funga ndoa jana jijini Dar Tunawatakia maisha Mema

Maharusi wakitabasamu kwa raha zao jioni ya leo kwenye moja ya ufukwe jijini Dar wakati wa foto shoot,mara baada ya kufunga ndoa katika kanisa la St.Anna,Hananasifu Kinondoni.
Wapambe wa maharusi wakiwa katika picha ya pamoja nje ya kanisa mara baada ya maharusi kufunga ndoa jioni ya leo.

Maharusi,Braza Cathbert Kajuna na Dada Easter Ulaya wakionesha shahada zao za ndoa mbele ya ndugu,jamaa na marafiki (hawapo pichani) walioshuhudia tukio hilo adhimu jioni ya leo ndani ya kanisa la St Anna,Hananasifu Kinondoni jijini Dar.Pichani nyuma ni Meneja Mahusiano wa kampuni ya Airtel,Jaskson Mmbando pamoja na Mkewe wakiwapa tafu maharusi.


Bibi Harusi,Da'Easter Ulaya akitabasamu kwa raha zake.
Maharusi wakionesha pete zao za ndoa mara baada ya kuvalishana.
Maharusi wakila kiapo cha ndoa.
"Alichokiunganisha Mungu,Mwanadamu asikitenganishe".!
Maharusi wakila kiapo cha ndoa.
Maharusi wakiwa kwenye ibada ya ndoa jioni ya leo.
Maharusi wakiingia kanisani,tayari kwa kuikamilisha ndoto yao ya kuisha pamoja,jioni ya leo huku wakisindikizwa ndugu jamaa na marafiki
(hawaonekani pichani).
Latest News Tz na uongozi mzima unawatakia maisha mema.

No comments: