Friday, September 16, 2011

LATEST UPDATES: TUKIO MAALUM LA AJALI YA MOTO ULIO WAKA LEO SOKO KUU LA SIDO MKOANI MBEYA LEO SEHEMU YA PILI



Moto ulianza pale majira ya asubuhi  Saa 3:50, lakini mpaka kufikia saa 5:15 Zimamoto walikuwa bado hawajafika na walipofika wakaaza kuzima moto ulikoanzia badala ya kule uelekeapo ili kunusuru mali nyingine zisiteketee.
 Na baadhi ya wafanyabiashara wamefanikiwa kuokoa bidhaa zao lakn waliowengi wamepata hasarA
Soko la Sido Mwanjelwa Jijini Mbeya ambapo chanzo cha Moto hiyo ni hitilafu ya umeme.
 Mto unaendelea kuteketeza bidhaa
Moto mkubwa ukiendelea kuwaka
 Masalia ya Bati zilizoteketezwa na Moto katika Soko la Sido.
 Gari la zima ambapo wananchi wakikinga maji kwa lengo la kusaidia kuzima maji vibanda vyao.
 Askari wa Jeshi la Kujenga Taifa JKT akiwa amemkamata mualifu ambaye alikuwa akijaribu kuiba bidhaa sokoni Hapo.
 Askari wa JKT wakimuadhibu mualifu au Kibaka
 Askari wa JKT na Polisi wakiwa wameweka chini ya Ulinzi kibaka.
Wezi na vibaka wafurahia tukio wakiwemo akina mama hili kwani imekuwa fursa kwao kutokana na kujinufaisha kwa kuiba ikumbukwe katika ajali iliyopita ya Soko la Mwanjelwa watu weki walipata mitaji kutokana na kuiba mali.

Moto ukiendelea kuchoma vibanda na makontena ya Biashara sokoni hapo.



Soko la mwanjelwa eneo la sido mbeya lawaka moto chanzo mapaka sasa hakijajulikana
Moto mkubwa ukiendelea kuwaka
Baadhi ya  mabanda sokono hapo tayari yameteketea kabisa na moto
Kama kawaida kikosi cha zimamoto mbeya kimeendelea na maigizo yake ya kuja kwenye tukio na gari bovu hapa wanaonekana askari wa kikosi hicho wakibishana huku moto ukiendelea 
Kufa kufaana kibaka tayari ameshaiba huyooo anatimka
Dada nae hayuko nyuma katika wizi keshachukua kapeti
Umati wa watu ukiwa unaangalia soko linavyoteketea
Mama huyu akilia kwa uchungu akiangalia duka lake likiteketea kwa moto
Mama  akiwa analia 
Hii ni hatari

No comments: