Kamati ya Miss Tanzania ilikaa na kutafakati kwa kuzingatia mambo yafuatayo:
1.Taarifa kamili ya maafa tulipata sa 9:30 mchana masaa machache kabla ya mashindano ya urembo ya Miss.Tanzania kuanza.
· Jibu letu:Ajali ilitokea saa saba za usiku,waokoaji walifika tokea saa kumi na mbili asubuhi,vyombo vya habari ulimwengu mzima vilitoa breaking news tokea saa mbili asubuhi na pia maandishi ya breaking news yalikua yanapita tokea saa mbili asubuhi takriban dunia nzima BBC,SKY NEWS,CNN,ALJAZIRA,N.K
· Kusema kwamba taarifa mliipata saa tisa kwa Tanzania si kweli sisi wa Ugiriki tumepata taarifa kupitia BBC saa nne asubuhi tena baada ya kuambiwa na raia wa kigiriki kuwa kumetokea maafa na ndio tukaamua kuangalia TV.
2.Wenzetu wa TFF waliendelea na mechi za ligi kuu ikiwemo Yanga na Ruvu Shooting.
Jibu letu: Haya ni mawazo finyu,hata mtoto wa darasa la tatu hawezi kusema kuwa nimetoroka shule kwa kuwa rafiki yangu nae ametoroka,ila atatoa sababu kama nilikua naumwa nilienda hospitali na sio sababu za kipuuzi,Kwa upande wa Biashara : Unahitaji kujua nini kuhusu washindani wako ambacho kitasaidia kuimarisha biashara je mlijiuliza masuala haya?
(a)Wao ni nani? (b)Hao TFF Wana biashara gani? (c) Wanapangaje bei za bidhaa zao? (d) Wana idadi ya wateja wangapi ukilinganisha na ya kwenu? (d) Kushindana nao kunaleta faida na hasara gani? (e) Kuingia kwanu katika soko au bidhaa au huduma zenu katika soko au kubadilisha bei zenu wanachukulia vipi?.
Utapata jibu kuwa biashara zenu ni tofauti kabisa hazihusiani na pia kushindana nao ni upuuzi kutokana wao wana objectives tofauti na zenu.
3.Kumbi za starehe na mabaa,burudani na mziki wa bendi kumbi za disco burudani
ziliendelea kama kawaida.
· Jibu letu:Ukiwachia kuwa wao wana objectives tofauti na nyie pia zingatia kuwa Mashindano ya Miss.Tanzania ni ya kitaifa,na yanaangaliwa karibu duniani kote lakini hakuna hata mmoja anaeangalia bar gani inauza vinywaji gani,(Service and Product industries are two different things) havihusiani.huwezi kabisa kuangalia wao wanafanya nini,ina maana wao wakitenda maovu na nyie mfanye pia?
4.Muda wa kuwakilisha mshiriki wa Miss.Tanzania kwenye Miss.World ulikuwa
umekwisha hivyo kulikuwa na hatari ya kukosa nafasi.
· Jibu:Hii ni very poor strategic planning,Kila biashara lazima itafakari kitaalamu kutumia PESTLE,(Enviromental analysis includes PUBLIC CONCERN) unahitaji ku asses biashara yako kama kweli inajali ethical and moral issues au kupata faida tu . tuchukue mfano ingelikua kumeripuka bomu ndani ya ukumbi mlioandaa mashindano yenu na washiriki wamefariki jee,mgelimchagua nani kuwakilisha?
· Lakini good strategic planning ni kwamba mngelichagua miss wenu kabla ya muda wa mwisho wa kuwakilisha kutokana kama kungetokea lolote kati ya hao mamiss basi mna muda wa kutosha kabisa kuchagua miss mpya na sio dakika ya mwisho,hiyo ni bad management kabisa.kwa kuwa planning ni kuondoa risk kwa hiyo mmeshindwa kulitambua hili na kujua thamani ya raia,ila mmejali faida tu.(Rais Kikwete ameandaa safari muda mrefu na gharama kibao na pia ni safari ya faida kwa Watanzania lakini amewacha safari hiyo ameamua kuenda kwenye msiba.)
5.Tamko rasmi la kusimamisha shuhuli zote za burudani kitaifa lilianza tarehe 11 september,
· Jibu:Sawa na iwe limetoka tarehe hiyo,je wewe ni binaadamu umepewa akili,sio kama mnyama ambae anaeweza kufanya mapenzi mbele ya watu, ina maana kama kungekua na moto barabarani ungeliendelea kupita hapo hapo tu,kwa kuwa hujaambiwa usipite kuna moto? Si ungelitumia akili yako kuwa utaathirika? Na vipi wale waliojitolea kuokoa walikua wasubiri tamko la serikali wakaokoe?
Mwisho tunapenda kumfahamisha bwana Mkubwa kuwa sababu zote zilizoorodheshwa ni very poor kwanza hazihusiani kabisa katika mazingira ya kibiashara pili zimeendelea kuwapa maumivu Watanzania,Tatu inaonekana hata shule ya management bwana mkubwa hajapitia,na Nne inaonekana wanajali maslahi yao tu na sio ya Taifa.
IT Manager (Abdul)
Vijana wa Kitanzania Ugirikia
1 comment:
Nimekubaliana na haya mawazo.Kama wangekua kweli na nia ya kuomba radhi wangeomba radhi tu, sababu walizotoa hazina mahusiano na kilichotokea
Post a Comment