Wednesday, September 7, 2011

MITIHANI YA DARASA LA SABA IRINGA......WANAFUNZI 1035 LUDEWA WAISHIA KTK UVUVI ZIWA NYASA

Wanafunzi wa darasa la saba katika shule ya msingi Muungano katika Halmashauri ya Manispaa ya Iringa wakiwa wamebeba vifaa mbali mbali vya kutayarishia chakula dakika chache kabla ya saa 10 jioni baada ya kula chakula cha pamoja mara baada ya kumaliza siku ya kwanza mitihani ya Taifa ya darasa la saba ambapo kwa leo wanafunzi hao walifanya mtihani wa Kiswahili , Hisabati na Sayansi ,mitihani hiyo kuendelea kesho
WANAFUNZI 1035 kati ya wanafunzi 5557 walioanza darasa la kwanza mwaka 2005 katika shule za msingi wilayani Ludewa mkoani Iringa wameshindwa kuungana na wanafunzi wenzao nchini kufanya mtihani wa kuhitimu elimu ya msingi ulioanza leo

Afisa elimu wa wilaya ya Ludewa Robert Hyera alimeueleza mtandao huu wa www.francisgodwin.blogspot.com kuwa wanafunzi 5557 ndio ambao waliadikishwa darasa la kwanza mwaka 2005 ila hadi leo ni wanafunzi 4522 pekee ndio ambao waliandikishwa kufanya mtihani huo wa kuhitimu elimu ya Msingi.

Hata hivyo alisema kuwa kati ya wanafunzi hao ambao wameanza mtihani leo wavulana ni 2160 na wasichana ni 2362 na kuwa hadi sasa zoezi la ufanyaji wa mkitihani hiyo kwa wilaya ya Ludewa linakwenda vizuri kutokana na maandalizi yote kwenda vizuri zaidi.

Pasipo kueleza sababu za wanafunzi hao 1035 kushindwa kumaliza elimu ya msingi bado afisa elimu huyo alisema kuwa ofisi yake itakuwa na jibu zuri zaidi baada ya zoezi hilo la mitihani kumalizika kesho

Afisa elimu huyo alisema kuwa pamoja na changamoto mbali mbali zinazoikabili wilaya hiyo ya Ludewa katika sekta mbali mbali hasa ya miundo mbinu ila bado wizara ya elimu imeweza kuhakikisha mitihani inafikishwa kwa wakati hadi katika shule za mwambao mwa ziwa nyasa ambazo kimsingi ndizo zilizo katika mazingira magumu ya kufikika kirahisi.

Ludewa ni moja kati ya wilaya ambayo wazazi walikuwa wakilalamikia watoto wao kufukuzwa shule kwa michango ya shilingi 600 za mitihani na hivyo wengi kujiunga na uvuvi wa samaki Ziwa nyasa hali iliyoshuhudiwa pia na mtandao huu kuona wanafunzi wakivua ziwani.

Wanafunzi wa darasa la saba leo wamefanya mtihani wa Kiswahili, Hisabati na Sayansi ambapo hadi sasa bado ofisi ya elimu mkoa wa Iringa bado haijasema chochote juu ya zoezi hilo kama limekwenda vema ama kuna uchakachuaji wa mitihani.
Na Francis Godwin

No comments: