Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi Nape Nnauye (aliyevaa pama) akizungukwa na wafanyabiashara katika soko la Igunga baada ya kupita karibu na soko hilo, akiwa katika matembezi yake ya kawaida katika mji wa Igunga mkoani Tabora leo.
Katibu wa NEC, Itikati na Uenezi CCM, Nape Nnauye akimvalisha kofia yake ya pama, mfanyabiashara katika Soko la Igunga, Joseph Kashinde baada ya mfanyabiashara huyo mwenye bendera ya CHADEMA kwenye banda lake la biashara (pichani) kuomba kuvaa kofia hiyo, Nape alipita katika soko hilo na kuzongwa kwa furaha na wafanyabiashara katika soko hilo leo.
Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi (CCM) Nape Nnauye (wapili kulia) akitoa pole kwa familia ya mtoto Peter Ezekiel nyumbani kwa wazazi wa mtoto huyo, Igunga mkoani Tabora leo. Mtoto huyo alifariki papo hapo baada ya kugongwa na lori la mizigo alipojaribu kukatiza barabara akitokea katika umati wa wananchi waliokuwa wakisubiri msafara wa mgombea wa ujumbe Igunga kwa timekti ya CCM, Dk. Dallally Peter Kafumu. CCM ilisimamia msiba huo hadi mazishi ambapo juzi wakati wa mazishi hayo ilitoa rambirambi ya Sh. milioni moja na Chadema sh. 120,000. Kulia Joseph Mlewa, Msemaji wa familia ya mtoto huyo,
No comments:
Post a Comment