Sunday, September 4, 2011

NGUMI KUPIGWA MWANANYAMALA JUMAPILI HI

Mratibu wa mpambano usio na ubingwa Ibrahim Kamwe katikati akiwainua mikono juu mabondia Bakari Mohamed (kushoto) na Ramadhani Shauli wakati wa kutangazwa kwa mpambano wao utakaofanyika jumapili hii
Bakari Mohamed kushoto wakitambiana na Ramadhani Shauli
Bondia Bakari Mohamed akipima uzito Dar es salaam jana kwa ajili ya mpambano wake na Ramadhani Shauli (kushoto) anashughudia kulia ni mratibu wa pambano hilo Ibrahim Kamwe (picha na
www.superdboxingcoach.blogspot.com)
MABONDIA Ramadhani Shauri na Bakari Mohamed 'Dunda' wanatarajia kupanda jukwaani katika pambano lao lisilo la ubingwa litakalofanyika katika ukumbi wa CCM Mwinjuma, Mwananyamala A, Dar es Salaam jumapili
hii..Pambano hilo linatarajia kuwa katika uzito wa kg 57 likiwa katika raundi nane ambapo pia litapambwa na burudani ya muziki wa asili kutoka katika kundi jipya la Makhirikhiri la hapa nchini.


Akizungumza Dar es Salaam leo, baada ya kupima uzito bondia Shauri alisema anajiamini kwa maandalizi aliyoyafanya kuwa yatamuwezesha kumtwanga mpinzani wake katika raundi za mwanzo na kuibuka bingwa."Nina maandalizi ya kutosha na ninaimani nitamtwanga Dunda kwani na jiamini na hawezi kunifikia kiuwezo," alisema Shauri.Naye kwa upande wake Dunda alisema, majibu ya tambo za mpinzani wake
huyo yatapatikana ulingoni hivyo mikono yake ndio itatoa majibu ya
majigambo yake yote.

"Siwezi kubishana kwa maneno kwani wakati nafanya mazoezi viungo vyangu hasa mikono ndio vilikuwa vinatumika hivyo naviacha vitende kazi yake," alisema Dunda.Hata hivyo mratibu wa pambano hilo Ibrahim Kamwe 'Bigright' alisema taratibu zote za kimaandalizi zimeishakamilika kwani siku hiyo
kutakuwa na ulinzi wa kutosha ambapo pambano litafunguliwa na burudani kutoka katika kundi hilo la Makhirikhiri.

Aliyataja mapambano mengine ya utangulizi kuwa ni Athony Mathias ambaye ataumana na Shabani Madilu, Joseph Mbowe na Ezekiel Juma ambapo Issa Omary ambaye atapigana na Kade Khamis huku mapambano haya yakiwa katika raundi nane,Katika raundi sita watakuwa ni Saadat Miyeyusho akichapana na Herman
Richard, huku raundi nne wakidundana Yona Miyeyusho na Haruna Said,Martin Richard na Jumanne Kilumbelumbe na Mwaite Juma akiwa na Frank Pury.

Wakati huo huo Kocha wa klabu ya ngumi ya Ashanti na Timu ya Mkoa wa Ilala ,Rajabu Mhamila 'Super D' atasambaza kanda zinazotoa mafunzo ya mchezo huo katika pambano hilo.Kutakuwa na uuzwaji wa DVD zenye mapambano ya mabingwa wa Dunia akiwemo Manny Paquaio, Floyd Maywherth, Roy Jones na wengine kiba DVD hizo zilizoandaliwa kwa ubora wa hali ya juu zitakuwa zikiuzwa kwenye mpambano huo na Kocha Rajabu Mhamila 'Super D', alisema kuwa kutakuwa na DVD ili kuweza kuwauzia mashabiki kwa ajili ya kujifunza Kanuni na Sheria za mchezo huo."Ninatarajia kuwapelekea DVD mashabiki wa ngumi watakaokuwepo katika pambano la Cheka na Maugo ili kuweza kujifunza mambo mbalimbali ikiwa ni pamoja na sheria za mchezo wa ngumi",
alisema Super D

No comments: