Friday, September 2, 2011

TBL Yachangia Vifaa Vya Maabara Na Ununuzi Wa Gari La Shule


Waziri Mkuu mstaafu, Cleopa Msuya (kushoto) ambaye pia ni Mwenyekiti wa Bodi ya Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), akipatiwa zawadi ya picha na wanakamati wa mahafali ya kumi ya Shule ya Sekondari ya St. Mary Goretti ya mjini Moshi juzi,kwa kutambua mchango wake wa maendeleo katika Taifa. katika mahafali hayo ambayo Msuya alikuwa mgeni rasmi, TBL, ilitoa msaada wa sh. milioni 10 za kusaidia kununua vifaa vya maabara na gari la shule hiyo.



Meneja Mauzo wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL),Mkoa wa Kilimanjaro, Leiya Hermenegild (kushoto) akimkabidhi mfano wa hundi ya sh.mil.10, Mkuu wa Shule ya Sekondari ya St. Mary Goretti ya mjini Moshi, Mtawa Lucretia Njau. Fedha hiyo ilitolewa na TBL kuchangia fedha za kusaidia kunua vifaa vya maabara na gari la shule hiyo. Hafla hiyo ilifanyika juzi wakati wa mahafali ya shule hiyo, ambapo Mgeni rasmi alikuwa Waziri Mkuu mstaafu, Cleopa Msuya ambaye pia nia Mwenyekiti wa Bodi ya TBL.

No comments: