CHAMA Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimepata wanachama wapya zaidi ya 50 kutoka Chama Cha Mapinduzi (CCM) wilayani Mbarali akiwemo aliyekuwa kada wa CCM kutoka kikosi cha Green Gurd Bw.Ayub Mlwilo huku wengine 138 wakijiunga na chama hicho.
Mwandishi wa mtandao huu kutoka Mbeya Esther Macha anaripoti kuwa Mavuno hayo ya chadema yalitokana na mkutano mkubwa ulifanyika juzi katika maeneo tofauti Wilayani Mbarali ambapo pamoja na masuala mengine kukusanya changamoto mbalimbali zinazowakabili wananchi wa maeneo hayo.
Akiwapokea wanachama hao wapya Mwenyekiti wa Wilaya Mbeya mjini Bw.John Mwambigija
aliwataka wanachama wapya kusoma ilani ya chama na kuielewa ili wasiwe watu wa kuhangaika kwenda vyama vingine visivyokuwa na ilani zinazotekelezeka.
“Sisi Chadema tunatekeleza yale ambayo tumeayaandika,tulisema tutakuwa tukiwashirikisha wananchi wetu mambo mbalimbali yanayowahusu na kutaka ushauri kwao ndicho tunachofanya leo”alisema .
Aidha Bw.Mwambigija aliwaeleza wananchi kuwa inapotokea baadhi ya watu hasa walio ndani ya chama tawala (CCM) kutekeleza matakwa ya wananchi hawa hutwa wasaliti na kuundiwa kesi zisizokuwa na ukweli wakidaiwa kuwa wafuasi wa Chadema.
“Hivi karibuni tu wananchi wa Mbarali mlishuhudia kukamatwa kwa mbunge wenu na hata kuwepo kwa ugumu wa Mdhamana mahakamani, hii yote ni njama ya CCM kwa kuwa mtu huyu anauchungu na maisha ya wananchi wake kiasi cha kusimamia kikamilifu mambo ya msingi ya wananchi,ajabu hawa CCM wanamwita mtu wa Chadema”alisema.
Hata hivyo Mwenyekiti huyo alimtaka Mbunge huyo kuachana na siasa uchwara,za kinafiki za CCM kwa kukiacha chama hicho na kujiunga na Chadema ili aweze kutimiza ndoto zake za kuwatetea wananchi wake katika kuhakikisha wanapiga hatua ya kimaendeleo hususani suala zima la umilikaji ardhi suala linalomletea misukosuko hivi sasa.
Baadhi ya wanachama waliojiunga na Chadema wakitokea CCM walisema kuwa waliamua kuchukua uamuzi wa kuihama CCM kutokana na kuonekana dhahiri kwa mazingira ya CCM kutaka kumwangamiza mbunge wao ambaye wanaamini ndiye mtetezi wao kwa kumuundia tuhuma zisizo na ukweli
No comments:
Post a Comment