Saturday, October 15, 2011

MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL AKUTANA NA MAMA MARIA NYERERE KIJIJINI BUTIAMA

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Mohammed Gharib Bilal kushoto, akizungumza na Mama Maria Nyerere wakati wa Chakula cha mchana kilichoandaliwa na Familia ya Baba wa Taifa Hayati Malimu Julius Nyerere baada ya kumalizika misa maalum kwa ajili ya kumkumbuka Baba wa Taifa pamoja na uwashaji mwenge wa Uhuru iliyofanyika katika kijiji cha Butiama jana. Katikati katibu wa Organaizeshen ya CCM Asha Abdalla Juma.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Mohammed Gharib Bilal na Mama Maria Nyerere katikati, wakiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa ujumbe uliomuwakilisha Rais Yower Museven wa Uganda kwenye Misa maalum ya kumkumbuka Baba wa Taifa Hayati Mwalim Julius Nyerere iliyofanyika jana kijijini kwake Mwitongo Butiama.
Mbunge wa Musoma vijijini Mhe. Nimrold Mkono akijumuika na wasanii wa ngoma ya asili ya mkoa wa Mara kucheza ngoma hiyo, wakati wa sherehe ya kuwasha mwenge iliyofanyika jana katika kijiji cha Butiama mkoani Mara jana.
Vijana wa Halaiki kutoka Shule za mikoa mbalimbali ya Tanzania wakifanya Halaiki ya onesho la kijeshi wakati wa sherehe ya kuwasha mwenge iliyofanyika jana katika kijiji cha Butiama mkoani Mara.
Amour Nassor VPO.

No comments: