Friday, October 21, 2011

MWENYEKITI WA WAMA MAMA SALMA KIKWETE AKUTANA NA UJUMBE WA G E CORPORATE KUTOKA MAREKANI

Picha ya pamoja baada ya Mwenyekiti wa Taasisi ya WAMA na Mke wa Rais Mama Salma Kikwete kumaliza mazungumzo na ujumbe kutoka Marekani pamoja na ungozi wa Wizara ya Afya na Ustawi wa jamii
Mama Salma Kikwete akiongea na wageni baada ya kumaliza mazungumzo.
Katibu wa Taasisi ya WAMA Daudi Nasibu (kulia) akiagana na Mjumbe kutoka Marekani wa Taasisi ya E G Health (kushoto) Reza Bundy baada ya kumaliza mazumgumzo na Mwenyekiti wa Taasisi ya WAMA Mama Salma Kikwete, (pichani hayupo) Mazungumzo hayo pia yamewahusisha wataalamu kutoka Wizara ya Afya na Ustawi wa jamii wakiongozwa na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Blandina Nyoni hayupo pichani.
Mwenyekiti wa Bodi ya Taasisi ya WAMA Zakhia Mehgji (kulia) akibadilishana mawazo katika ofisi za WAMA jijini Dar es Salaam na wajumbe wa taasisi ya E G Health kutoka Marekani (kushoto)ni Director, Global Programs healthymogination Joneen Uzzeli na (aliesimama katikati) ni Co- Director of African First Ladies Fellowship Program Cora Neumann, wakati ujumbe huo ulipokwenda kumtembelea Mwenyekiti wa Taasisi hiyo Mke wa Rais Mama Salma Kikwete (hayupo pichani ) na kuzungumzia jinsi ya kusaidia kuwaletea vifaa tiba kwaajili ya kusaidia kupunza vifo ya wakinamama na watoto wachanga nchini .
Katibu wa Taasisi ya WAMA Daudi Nasibu (aliesimama) akitoa taarifa kwa wageni pamoja na uongozi wa Wizara ya Afya na Ustawi wa jamii katika Ofisi za WAMA walipokutana na Mke wa Rais na Mwenyekiti wa Taasisi hiyo Mama Salma Kikwete kuzungumzia masuala mbalimbali kuhusu kusaidia kuleta vifaa tiba kwaajili ya jitihada za kupunguza vifo vya wakinamama na watoto wachanga nchini.
Picha na Mwanakombo Jumaa-MAELEZO.

No comments: