Monday, October 3, 2011

Taarifa Mpya: Mapanga Yavurumishwa Igunga Asubuhi Hii

Kumetokea tukio la wafuasi wa vyama vikuu vya kisiasa vya CCM na CHADEMA kukabiliana na hata matumizi ya silaha za jadi kama mapanga katika rabsha hizo. Msomaji wa makala zangu anayefanya biashara ya kuchuuza samaki sokoni Igunga amenijulisha kwa simu kuwa amenusurika kupigwa panga alipokuwa akipita nje ya hotel ya Peak asubuhi hii. Kwa sasa yuko nyumbani kwake akifuatilia upepo unavyokwenda. Wenye taarifa zaidi ya kinachoendelea Igunga watujuze.
Taswira na Mjegwa Blog

No comments: