Tuesday, October 4, 2011

Tanga Cement Kusaini Makubaliano Ya Ushirikiano (MoU) Na Chuo Cha Ufundi Arusha

Mkuregenzi mkuu wa TCCL Bw Erik Westerberg (kushoto) akiweka saini ya Ushirikano (MoU) kati ya Chuo cha ufundi Arusha na Tanga Cement. Kulia kwake ni Mkuu wa Chuo cha Ufundi Arusha Dkt Richard Masika.
Mkuregenzi mkuu wa Tanga Cement Bw Erik Westerberg akizungumza mara baada ya kutia saini makubaliano ya Ushirikano (MoU) kati ya Chuo cha ufundi Arusha na Tanga Cement.

Kampuni ya saruji Tanga(TCCL) imesaini makubaliano ya Ushirikano (MoU)
na Chuo cha Ufundi Arusha (ATC) kwa lengo kukuza weledi na umahiri wa
ufundi katika matumizi ya saruji Tanzania.


Katika makubaliano hayo, Kampuni ya saruji Tanga Itaipa ATC tani 2 za
saruji kila baada ya miezi mitatu kwa ajili ya mafunzo kwa vitendo
kwa hasa kwa wanafunzi wanasoma programu ya mhandisi Ujenzi. Pia
itasaidia chuo katika matengenezo ya vifaa vya kupimia uimara wa
bidhaa za saruji pamoja utafiti wa bidhaa za saruji.
Picha Gesto Leseiyo

1 comment:

Anonymous said...

Hongera Tanga Cement. Makampuni mengine nayo twigs mfano huu ili vyuo viwe na uwezo wa kutoa wahitimu mahiri! Big uuuup TCCL!!