Thursday, October 13, 2011

Wizara ya Habari,Vijana,Utamaduni na Michezo Wamtembelea Mama Maria Nyerere Butiama Mkoani Mara


Naibu Waziri wa Habari,Vijana, Utamaduni na Michezo, Dkt. Fenella Mukangara akimpatia kitabu cha taarifa ya miaka 50 ya uhuru wa Tanzania Bara kwa Wizara hiyo leo nyumbani kwa Mjane wa Hayati Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere, Mama Maria Nyerere mara baada ya kumtembelea nyumbani kwake Butiama, mkoani Mara.
Mjane wa Baba wa Taifa, hayati Mwalimu Julius Nyerere, Mama Maria Nyerere akizungumza na Naibu Waziri wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dk. Fenella Mukangara wakati alipombelea nyumbani kwake kijijini Butiama, mkoani Mara leo (jana). Kulia kwa Naibu Waziri ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Bi Sihaba Nkinga pamoja na Viongozi waandamizi wa Wizara hiyo.
Mtoto wa Hayati Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere, Makongoro Nyerere akitoa historia ya makaburi ya wazazi wa mwalimu Julius Nyerere yaliyopo mwitongo, Butiama kwa Viongozi waandimizi wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo waliokwenda kumjulia hali Mama Maria Nyerere.
Mkuu wa Mkoa wa Mara (kulia) John Tupa akipata maelezo juu ya majukumu ya Idara ya Habari (Maelezo) kutoka kwa Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Habari (Maelezo) Ndg. Raphael Hokororo mara baada ya kutembelea banda la Idara hiyo katika maonyesho ya maadhimisho ya miaka 50 ya uhuru wa Tanzania Bara kwa Wizara hiyo yanayoendelea katika uwanja wa kumbukumbu ya Joseph Kazurira Nyerere, huko Butiama mkoani Mara.
Mkuu wa mkoa wa Mara John Tupa(katikati) akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) katika banda la Idara ya Habari kuhusiana na maandalizi ya mbio za mwenge wa uhuru unaotarajia kuwashwa mkoani humo. Wa pili kushoto ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Bi. Sihaba Nkinga na kwanza na kwanza kushoto ni kaimu Afisa Utamaduni na Michezo, Shekheadi Saidi. Wengine wa pili kulia ni Katibu Tawala wa Mkoa huo, Clement Lujaji na wa kwanza kulia ni Mkurugenzi mtendaji wa Wilaya ya Musoma, Dkt. Karaine Kimaati.
Naibu Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Fenella Mukangara mara baada ya kumtembelea Mjane wa Mwalimu Nyerere, Mama Maria Nyerere kijijini kwake Butiama, mkoani Mara leo. Wengine katika picha ni Viongozi waandamizi wa Wizara hiyo, kulia hiyo ni mtoto wa Hayati Baba wa Taifa, Madaraka Nyerere.Picha Zote na Anna itenda-MAELEZO

No comments: