Friday, November 18, 2011

KUTOKA VIWANJA VYA BUNGE LEO MJINI DODOMA



Mbunge wa Mbeya mjini (Chadema) Joseph Mbilinyi akibadilishana mawazo
na Mbunge wa Nkenge (CCM) Bi. Asumpter Mshama nje ya ukumbi wa Bunge
mjini Dodoma leo mara baada ya kumalizika kwa kipindi cha maswali na
majibu.



Katibu
Mtendaji wa shirikisho la filamu Tanzania, Wilson Makubi akitoa mada
katika semina elekezi kwa Maafisa utamduni wa Halmashauri mbalimbali za
wilaya nchini juu ya matumizi ya kanuni mpya za filamu na michezo ya
kuigiza. Semina ya siku mbili itafanyika katika ukumbi wa St. Gasper
mjini Dodoma na inatarajia kufungwa rasmi kesho tarehe 19/11/2011.



Mwanasheria wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Patrick Kipangula akitoa ufafanuzi kwa Maafisa Utamaduni kuhusu
vifungu vya kisheria vya kanuni mpya za filamu na michezo ya kuigiza
vilivyo wakati wa semina elekezi kwa maafisa hao inayofanyika katika
ukumbi wa St. Gasper mjini Dodoma. Semina hiyoinatarajia kufungwa kesho tarehe 19/11/2011.



Mbunge wa Mafia (CCM)Abdulkarim Shah akizungumza na baadhi ya wabunge
wa vyama vya upinzani vya NCCR mageuzi na CHADEMA nje ya ukumbi wa
Bunge mjini Dodoma leo mara baada ya kumalizika kwa kikao cha asubuhi.
Wa kwanza kushoto ni Mbunge wa Kigoma Kusini (NCCR Mageuzi) David
Kafulila anayefuatia ni Mbunge wa Nyamagana (Chadema) Ezekia Wenje na
katikati ni Mbunge wa Ksulu Mjini (NCCR Mageuzi), Moses Machali .Picha na Anna Itenda- Maelezo

No comments: