Monday, November 14, 2011

Mh.Godbless Lema aachiliwa huru mpaka Disemba kumi na nne

Na Gladness Mushi Arusha

Mbunge wa jimbo la arusha mjini Bw. Goodbless Lema leo ameachiliwa huru na mahakama ya hakimu mkazi mara baada ya kukidhi vigezo vya mahakama katika kesi ambayo inamkabili mbunge huyo ya kufanya maandamano na mkusanyiko bila kibali maalumu cha vyombo vya usalama.

Hayo yalikuja mara baada kudaiwa mahakamani hapo kuwa mtuhumiwa namba moja ambaye ni Mbunge wa jimbo la arusha mjini kuwa nje kwa dhamana hadi Disemba 14 mwaka huu

Aidha hakimu ambaye anasikiliza kesi hiyo Bi Judith Kamala aliiambia mahakama kuwa mtuhumiwa huyo kisheria yupo huru kwa kuwa vigezo vya mahakama vilidai kuwa mtuhumiwa huyo namba moja anatakiwa kuwa na wadhamini wawili jambo ambalo walikidhi vigezo
hata hivyo kesi hiyo iliahirishwa ambapo itasikilizwa tena mahakamani hapo Disemba 14 mwaka huu.

Katika hatua nyingine mbunge huyo aliambia vyombo vya habari kuwa
mkuu wa Mkoa wa Arusha Bw Magesa Mulongo anatakiwa kuacha ushabiki wa kisiasa na kama hataweza kuacha ushabiki huo atalazimika kuwatumia wanawake yaani mke wa mbunge na mke wa mkuu wa mkoa ili waweze kusuluishana.

Aidha Bw. Lema alisema kuwa hatua hiyo itakuja kwa kuwa mara nyingi mkuu huyo ameonekana akisema na kuwatetea chama cha mapinduzi hali ambayo inachangia unyanyasaji mkubwa sana

Aliongeza kuwa hali hiyo ya kumtuma mke wake kwenda kwa RC mkoa wa Arusha huenda ikaleta maafanikio zaidi kwa kuwa wanawake kwa wanawake wanaweza kusikilizana tofauti na wao ambao mpaka sasa tofauti zimeshajitokeza sana.

katika hatua nyingine Bw Lema aliongeza kuwa wananchi wanapaswa kujua na kutambau kuwa yeye si mwehu kukataa dhamana na badala yake wanatakiwa kujua kuwa anatafuta haki ambayo inaondolewa na baadhi ya vyama vya siasa pamoja na Jeshi la polisi

Alibainisha kuwa kwa kuwepo kwake Gerezani ameweza kugundua na kujua kuwa ndani ya jeshi la polisi wapo baadhi ya askari ambao wanakiuka taratibu za jeshi hilo na kuwapa watu kesi ambazo si za kwao hali ambayo inasabbaisha madhara makubwa sana kwa wananchi hasa wale wenye kipato cha chinil.

Bw Lema alisema kuwa wananchi wanatakiwa kuhakikisha kuwa wana kemea vibaya tabia ya kunyimwa haki zao za msingi na pia wananchi hao wana haki

Habari kwa hisani ya Full Shangwe Blog

No comments: