Wednesday, November 9, 2011

Mwenyekiti wa Chadema,Freeman Mbowe ajisalimisha polisi mkoani arusha leo

Mwenyekiti wa chama cha demokrasi na maendeleo (Chadema),Freeman Mbowe akiwasili kwenye Ofisi za Jeshi la Polisi Mkoani Arusha leo asubuhi kwa ajili ya kujisalimisha kufuatiwa kusakwa na Jeshi hilo kwa tuhuma za kuvunja sheria.
Mwenyekiti wa Chadema,Freeman Mbowe akiingia katika ofisi za mkoa za Jeshi la Polisi mkoni Arusha leo,aliyevaa nguo nyeusi ni Mbunge wa Viti Maalumu wa Chadema,Joyce Mukya akiwa amemsindikiza mwenyekiti wao kujisalimisha Polisi.
Mkuu wa Operation wa Jeshi la Polisi Mkoani Arusha,Saimon Pilo (kulia) akiwa amempokea Mwenyekiti wa Chadema,Freeman Mbowe (katikati) katika Ofisi ya Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha kwa ajili ya kufanya nae Mazungumzo,wakati Mwenyekiti huyo alipofika Kituoni hapo Kujisalimisha leo asubuhi.Kushoto ni Mbunge wa Viti Maalumu wa Chadema,Joyce Mukya alieongozana na Mwenyekiti wake.
Mwenyekiti wa Chadema,Freeman Mbowe akiwa anatafakari jambo ndani ya Ofisi ya Kamanda wa Polisi Mkoa Arusha leo.
Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema),Freeman Mbowe akitoka kwenye Ofisi ya Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha na kuelekea katika Ofisi ya Upelelezi Wilaya ambapo alielekezwa aende huko na Mkuu wa Operesheni wa Jeshi la Polisi Mkoani Arusha.
Picha zote na Woinde Shizza,Arusha.

1 comment:

Anonymous said...

...NAMPA MOYO ASIKATE TAMAA KWANI HATA BABA WA TAIFA J.K NYERE NA BABA WA AFRIKA KUSINI NELSON MANDELA KATIKA HARAKATI ZA KUDAI HAKI(UHURU) WA WATU WAO WALIPITIA MILIMA NA MABONDE KAMA HAYO(POLISI,GEREZANI,MABOMU YA MACHOZI,RISASI ZA MOTO,MAJI YA KUWASHA,MBWA WAKALI WA POLISI N.K).