Rais Jakaya Kikwete akimsalimu na kumpa pole mtoto Ali Abdul (13) kutoka Rufiji, mkoa wa Pwani, aliyetoka kufanyiwa upasuaji wa kuzibua mishipa ya damu iliyozibwa na madaktari bingwa toka India amabo wako nchini kusaidia kazi katika kitengo cha tiba ya figo katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili jijini Dar es salaam. Kitengo hicho kimeundwa mahususi kusaidia watu wa matabaka yote kupat matibabu ya figo ikiwa ni moja ya jitihada za serikali kusaidia wananchi wake kupata matibabu hayo hapa hapa nchini na kwa gharama nafuu. Rais Kikwete ameonesha kufurahishwa na kuridhishwa na maendeleo ya kitengo hicho ambacho muda si mrefu ujao kitakuwa na uwezo wa kutibu wagonjwa wengi zaidi.
Rais Jakaya Kikwete akisalimiana na mmoja wa wauguzi katika kitengo hicho.
Mkuu wa kitengo na daktari bingwa wa figo, Dk. Linda Ezekiel akimtambulisha Rais Jakaya Kikwete madaktari bingwa toka India wanaosaidia kazi katika kitengo cha tiba ya figo katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili.
Rais Jakaya Kikwete akiongea na madaktari bingwa hao toka India.
Rais Jakaya Kikwete katika picha ya pamoja na madaktari bingwa toka India na wa Tanzania aliowatembelea katika kitengo cha tiba ya figo katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili jijini Dar es salaam.(Picha na (http://ikulublog.com/)
No comments:
Post a Comment