Tuesday, November 29, 2011

TUKIO LA MAAFA LA MAFURIKO KARATU JANA




 Mwili wa marehemu Samweli Julius ambaye alikuwa ni msaidizi wa mitambo ya kutengeza barabara, ukiwa umenasa juu ya mti. 
 Mfanyakazi wa Mahakama ya Kimataifa ya Mauaji ya Kimbari ya Rwanda (ICTR), Augustino Masige, aliyekuwa akiendesha gari namba T573 AHW, akitoka Arusha kwenda Musoma, akisimama kando ya gari lake lilosukumwa na maji umbali wa mita 50 toka barabarani. 


 Lori la mizigo namba T190 AKW likiwa limebeba mitambo ya kutengeneza barabara likitoka Engaruka kwenda Arusha. 
  Hii ni nguzo ya umeme iliyopo maeneo hayo ambayo nayo wakati wowote yawezakuanguka. 
 Polisi walifika eneo la tukio na kufanya ugaguzi wa matukio hayo ya ajali. 
 Polisi wakatoa idhini sasa ya mwili wa Samweli kutolewa katika eneo ulipopatikana. 
 Njia hii ikafungwa nusu kuepusha maafa kutokea baada ya kipande cha barabara hiyo kumegwa na maji katika daraja la Mto Loobuko. 
 Hivi ndivyo kipande hicho cha barabara kilivyomegeka na maji. 


Hakika maafa yatokeapo hukumba kila kiumbe hai katika jamii. Mbwa huyu si kuwa aliathirika na mafuriko hayo bali alionesha uzalendo wake wa kweli na kufika katika eneo la tukio na kuangalia mwenyewe kilichojiri. 
Picha zote na mwakilishi wa Latest news Tz Francis Tumbo
  

No comments: