Saturday, November 12, 2011

Wafanyakazi wa kituo cha Radio Five watembelea Bungeni na kufanya mahojiano na Spika wa Bunge

Spika wa bunge la Jamhuri ya Muungano wa TanzaniaMh. Anne Makinda akifanya mahojiano na Mtangazaji wa Kituo cha Radio Five David Rwenyagira ofisini kwake mjini Dodoma. Mh. Makinda alikuwa akizungumzia mambo mbalimbali pamoja na changamoto za mwanamke wa Kitanzania.
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Mh. Anne Makinda akiwa katika picha ya pamoja na wafanyakazi wa kituo cha Radio Five walipofanya naye mahojiano ofisini kwake mjini Dodoma.Katikati ni David Rwenyagira, kulia ni Mohamed Hamis na kushoto ni Monika Nagu. Waliosimama nyuma mwenye suti nyeusi ni Mkurugenzi wa kituo hicho Robert Francis na wa nyuma ni Meneja wao Jimmy Mtemi.
Waziri wa Maendeleo ya Wanawake Jisnia na WatotoMh. Sophia Simba akipokea maelekezo kutoka kwa Mtangazaji wa Radio Five David Rwenyagira alipotembelea bungeni mjini Dodoma. Katikati ni Meneja wa radio hiyo Jimmy Mtemi,kulia ni fundi mitambo wa kituo Mohamed Hamis na anayeangalia kwa nyuma ni mtangazaji Monika Nagu.
Habari kwa hisani ya Michuzi Blog

No comments: