Monday, December 12, 2011

PIMA-MAJI YA MJENGWABLOG: GODBLESS LEMA AWATIMULIA VUMBI ZITTO NA MNYIKA!
Ndugu zangu,
Siku tano zimebaki za kupiga kura. Mchuano ni mkali. Ni katika mchakato huu wa kumpata mbunge bora Kijana kwa mwaka 2011.


Habari kubwa siku ya leo?


Ni ’ Kamanda’ Godbless Lema.


Anaongoza mbio kwa zaidi ya kura 25 mbele ya Zitto Kabwe.


’ Kamanda’ Lema kama anavyoitwa na wafuasi wake alianza mbio hizi akiwa kwenye nafasi ya tatu. Kuna wakati niliandika, kuwa ’ Mandela effect’ haikumsaidia. Nilikosea!


Ajabu ya Godbless Lema…


Hayuko active sana mtandaoni kama ilivyo kwa Zitto, Mnyika, Makamba na Dewji, lakini, katika siku tatu zilizopita ameweza kutoka nafasi ya tatu hadi ya kwanza.

Inaonekana, kuwa Lema ana ushawishi mkubwa na kwamba mji kama Arusha ambako anakubalika sana ’ wapiganaji’ wake wanaonekana kuwa organaized. Kuna ambao wana uwezo wa kipato pia, kwamba wana fursa ya kutumia teknolojia ya kisasa kumpigania Lema mtandaoni.Naam, Godbless Lema anaonekana kuwa na kura nyingi zilizoko ardhini na ambazo zinaweza kuingizwa mtandaoni kwa kusaidiwa na organaization ya ardhini. Kwamba hata kama huko nyuma John Mnyika na Zitto Kabwe wameonekana kutawala mitandaoni, lakini, wapiganaji wao wa mitandaoni wameanza kumalizika. Ili kura zao zitoshe mwisho wa siku, basi, wafuasi wao wa mitandaoni watakuwa na lazima ya kujipanga upya. Maana, Godbless Lema anakuja na moto.


Ilivyo sasa:


Kura mia nne zimepigwa jana. Ni ongezeko la kura mia kutoka wastani wa kura mia tatu kwa siku. Jumla ya kura elfu mbili zinatarajiwa kuwa zimepigwa ifikapo jioni ya leo. Ni idadi kubwa ya kura katika kipindi kifupi kinyume na ilivyotarajiwa. Tafsiri? Hamasa ya mchakato huu imeongezeka. Idadi ya wanaoelewa mantiki ya zoezi hili inaongezeka. Ukiacha wanaopuuza huku wakifuatilia kila siku, kuna wanaona umuhimu wa mchakato huu na kwamba kuna ya kujifunza kwa kura hizi za mtandaoni.


Zitto Kabwe:

Ni mwanasiasa mkongwe mtandaoni. Anasadikiwa kuwa na mtandao mpana unaoweza kuamua lolote katika mbio hizi. Juzi alikuwa nyuma ya John Mnyika, na jana alimpita Mnyika na kuna wakati alikuwa akiongoza mbio mbele ya Godbless Lema.Namna gani John Mnyika?Kasi ile aliyoanza nayo inaonekana kupungua. Ameteremka hadi nafasi ya tatu. Ni

Ni mapema mno kuhukumu mwenendo wa Mnyika. Tuko kwenye mapumziko ya mwisho wa juma na Ijumaa ilikuwa siku ya sikuu. Mnyika, kama ilivyo kwa Zitto, wana wapiganaji wao walio maofisini. Jumatatu ya kesho inaweza kutoka sura nyingine ya mtanange.Mr. Sugu:

Alichonacho Godbless Lema yawezekana Mr. Sugu hana, wapiganaji waliojipanga ardhini kuweza kurusha ‘ makombora’ ya kura mtandaoni. Na kwa sasa tishio kwa Sugu sio tu January Makamba, bali hata ’ Mo’ Dewji anaweza kupambana na kumfikia Sugu.January Makamba:

Makamba anazungumza na anazungumzwa mtandaoni. Hivyo basi, kura zake zinaongezeka na anabaki kuwa mbunge nyota kijana ndani ya chama chake kwa sasa.’Mo’ Dewji na ’ Kiduku effect!


Kuna wanaompenda ’ Mo’ Dewji kwa jinsi alivyo pia. Kwenye jamii anaonekana hana makuu. Huo ni mtaji muhimu kwa mwanasiasa. Kwenye kucheza ’ Kiduku’ yumo kwenye kushangilia Taifa Stars yumo, tena tumbo wazi! Na jimboni kwake ana vya kuonyesha kuwa amefanya. Kwa nini akose kura?Akina Mkosamali na wenzake wameanza kuokoteza kura njiani
Tumeona jana, kuwa Mkosamali na Serukamba wameokoteza njiani kura moja moja na kuziingiza kapuni. Kila mmoja sasa ana kura mbili. Ushauri kwa wabunge vijana. Huko kwenye vyuo vikuu yumkini kuna wanafunzi waliotokea kwenye majimbo yao. Wawe wanakwenda kuongea nao. Ndio mwanzo wa kuongeza kura mitandaoni.

Naam, siku ya leo nayo inaweza ikazaa habari mpya kesho. Nenda sasa www.mjengwablog.com kupiga kura yako. Mahali ni juu kulia.Maggid Mjengwa,

Mratibu.

Iringa,
No comments: