Thursday, December 1, 2011

Rais Jakaya Kikwete Akabidhi Mwenge Wa Uhuru Jeshi La Wananchi Wa Tanzania ili Upandishwe Kwenye Kilele Cha Mlima Kilimanjaro

Viongozi wa wataopandisha mwenge wa Uhuru mlima kilimanjaro
Rais Jakaya Kikwete baada ya kuuopokea mwenge wa uhuru
Rais Kikwete akipokea mwenge wa uhuru kutoka kwa kiongozi wa mbio hizo mwaka huu
Rais Jakaya Kikwete akimkabidhi mwenge wa uhuru mkuu wa majeshi Jenerali Davies Mwamunyange ambaye atawakabidhi wapandishaji mlima kilimanjaro
Rais Jakaya Kikwete akiwatakia heri Mkuu wa Majeshi ya Tanzania Jenerali Davies Mwamunyange na wanajeshi wataopandisha kilele cha mlima Kilimanjaro Mwenge wa Uhuru mkesha wa siku ya uhuru. Kushoto ni Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dkt Emmanuel Nchimbi , wa pili kulia ni Naibu waziri katika wizara hiyo Dkt Fenella Mukangara na wa kwanza kushoto ni mmoja wa wataopandisha Mwenge mlima Kilimanjaro.
Mkuu wa Mkoa wa Tabora Mh Fatuma Mwassaakipokea kikombe cha ushindi kutoka kwa Rais Jakaya Kikwete
Rais Jakaya Kikwete akikabidhi mfano wa hundi ya shilingi milioni moja kwa Mkuu wa Mkoa wa Tabora Mh Fatuma Mwassa na maafisa wake baada ya mkoa huo kuibuka mshindi wa jumla wa mikoa iliyofanya vyema katika mbio za mwenge wa wingi wa miradi na maandalizi.
Rais Jakaya Kikwete akihutubia katika maadhimisho ya kilele cha mbio za Mwenge wa Uhuru leo Uwanja wa Uhuru jijini Dar es salaam. Walioketi toka kulia ni IGP Saidi Mwema, Mkuu wa Majeshi Jenerali Davies Mwamunyange, Spika wa Bunge Mh Anne Makinda
Mama Maria Nyerere na Mama Salma Kikwete na wageni wengine mashuhuri jukwaa kuu.
Rais Jakaya Kikwete akipokea maandamano ya kilele cha mbio za mwenge
Sehemu ya umati wa watu
kikosi cha wataopandisha mwenge wa uhuru mlima kilimanjaro.
Picha Zote na IKULU



No comments: