Sunday, December 18, 2011

RAIS KIKWETE AREJEA NCHINI, AKABIDHI NISHANI YA DR WILBERT CHAGULA KAMPALA LEO...!!!


Rais Jakaya Kikwete akiwa na mazungumzo na Makamu wa Rais Dr Mohamed
Ghalib Bilal na Waziri Mkuu Mh Mizengo Pinda mara baada ya kurejea
jijjini Dar es salaam kutoka Kampala, Uganda, alikohudhuria mkutano wa
siku mbili wa wakuu wa nchi za maziwa makuu


Rais Jakaya Kikwete akiagwa na Kaimu Balozi wa Tanzania nchini
Uganda, Mh Nsavike G. Ndatta katika uwanja wa ndege wa Entebbe leo
Desemba 17, 2011 asubuhi wakati akiondoka Uganda kurejea nyumbani baada
ya kuhudhuria mkutano wa siku mbili wa wakuu wa nchi za maziwa makuu
Rais Jakaya Kikwete akiwakabidhi Bw. Clement A. Chagula na bintiye
Olivia A. Chagula medali kwa niaba ya baba na babu yao Marehemu Dkt.
Wilbert Chagula, ambaye aikuwa ni mmoja wa mawaziri katika serikali ya
awamu ya kwanza na mmoja wa watu maarufu waliotunukiwa nishani katika
kuadhimisha miaka 50 ya Uhuru. Bw Chagula, ambaye ni mtoto wa marehemu,
hakuweza kufika Dar es salaam kupokea medali hiyo na Rais alipokuwa
Kampala akatumia nafasi hiyo kumpatia leo asubuhi katika hoteli ya
Speke. Commonwealth Resort

(PICHA NA IKULU)


No comments: