Thursday, December 1, 2011

Unaringa Umepima!!?..... Huwezi kumtambua Aliye athirika kwa kumwangalia usoni kwani Hawana alama

Tumeanza na Kauli kwamba Unalinga Umepima?.... Na tukamalizia kwa kusema kwamba huwezi Mtambua kwa macho kwani Hawana Alama.. Ni ujumbe ambao Tunapenda Kuwafikishia Nyote katika siku ya leo ya UKIMWI Duniani ambapo watu wote tunakumbuka jinsi maambukizi yanavyo tishia amani na watu wanavyo teseka pia kuwakumbuka wale woote ambao wametutoka, Poleni Nyote ambao mmetokwa na Ndugu zenu walio Athirika kwa UGONJWA huu ambao tunaweza sema sio wa Hatari lakini ni Ugonjwa wa Mateso Makubwa sana. Hivyo basi Tunapaswa kuwa makini sana.

Katika Kuadhimisha siku hii ya Leo Tunawasihi Ndugu Zetu nyote kwamba kuwa makini maana wengi wetu hasa wanandoa mmekuwa hamtulii sana na familia zenu na kwenda nje kufanya mambo mengine na kurudi nyumbani kumwambukiza mwenzio ugonjwa.. Hii ni kweli na imethibitika wanandoa wengi ndio chanzo kikubwa cha Maambukizi ya Ugonjwa huu. hivyo tuwe makini.

Kundi la pili la maambukizi ni wale ambao wanajua wameathirika na wanataka kutumia mabavu ya pesa zao kuendelea kusambaza virusi hivyo vya ukimwi, Katika siku ya leo ya kilele cha siku ya Ukimwi Duniani Tunakemea vikali kabisa na kuwaomba wale wote tunao wajua watu wenye tabia hizi za kufanya maambukizi kwa makusudi kukemea viakali  kabisa ili kupunguza maambukizi haya ya Ugoinjwa wa Ukimwi.

Kundi la tatu ambalo sasa pia Linakuwa na waathirika wengi ni vijana wa mashuleni vyuoni na pia sekodari ambao pia wanakumbwa na balaa hili la maambukizi kwa kasi sana. Tunawaomba wote kuwa makini sana, na kwa wanafunzi wa Vyuoni tujiulize swali moja tuu, kwa nini Mfe mapema? na huku Taifa linawategemea? Basi tuchukue Tahadhari kabla ya hatari.

Kabla hatujamaliza Tunapenda kuipongeza sana Serikali ikiongozwa na Rais Mh. Jakaya Kikwete pale alipo sema Tanzania Bila Ukimwi inawezekana na imeleta matunda sana kauli Mbiu yake na maambukizi ya Ugonjwa huu yanaonekana Dhahili Kupungua kwa kasi kubwa.

TAFAKARI NA CHUKUA HATUA 



No comments: