Saturday, December 3, 2011

WAZIRI MWANDOSYA KATIKA MKUTANO NA WATENDAJI WAKUU WA WIZARA YAKE LEO

Waziri wa Maji, Profesa Mark Mwandosya wa pili kutoka (kushoto) akiwa na Katibu Mkuu wa wizara hiyo, Mhandisi Christopher Sayi wa pili kutoka (kulia) wakati akielekea katika ukumbi wa mikutano wizarani hapo kwa ajili ya kuzungumza na baadhi ya watendaji wakuu wa wizara na waandishi wa habari ili kutoa shukrani kwa watu mbalimbali waliokuwa wakimjulia afya yake na kumwombea. Na wa kwanza kutoka (kulia) ni Naibu Katibu Mkuu wa wizara hiyo, Bashir Mrindoko. Kushoto ni mtoto wa waziri, Emmanuel Mwadosya.
Waziri wa Maji, Profesa Mark Mwandosya (kulia ) akizungumza na viongozi watendaji wakuu wa wizara hiyo na waandishi wa habari kuhusu kutoa shukurani kwa watu mbalimbali waliokuwa wakimjulia afya yake na kumwombea, akiwemo Rais Jakaya Kikwete, Makamu wa Rais Dk. Mohamed Gharib Bilal ,Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, Spika wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Anne Makinda, viongozi wa dini na wa kisiasa ambao ni Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Maalim Seif Sharif Hamad , na Profesa Ibrahim Lipumba na wananchi Watanzania kwa ujumla bila kujali Itikadi za kisiasa. Kushoto ni Naibu Waziri wa wizara hiyo Gerson Lwenge .

Viongozi Watendaji Wakuu wa Wizara ya Maji na waandishi wa habari wakimsiliza kwa makini Waziri wa Maji, Profesa Mark Mwandosya wakati alipokuwa akitoa shukurani kwa watu mbalimbali waliokuwa wakimjulia afya yake na kumwombea, akiwemo Rais Jakaya Kikwete, Makamu wa Rais Dk. Mohamed Gharib Bilal ,Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Anne Makinda , viongozi wa dini na wengine wa kisiasa ambao ni Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Maalim Seif Sharif Hamad , na Profesa Ibrahim Lipumba na wananchi Watanzania kwa ujumla bila kujali Itikadi za kisiasa. Kushoto ni Naibu Waziri wa wizara hiyo Gerson Lwenge.
PICHA ZOTE NA KWA HISANI YA WIZARA YA MAJI.

No comments: