Saturday, January 28, 2012

Askari polisi wawili wapoteza maisha na wengine wanne kujeruhiwa katika ajali ya gari mkoani tanga

viongozi wa Serikali na wananchi wa kijiji cha Nduu,Mombo mkoani Tanga wakitafuta namna ya kuwatoa askari wa kikiso cha kutuliza ghasia (FFU) mkoani Tanga mara baada ya gari lao lenye namba za usajiri PT 2000 aina ya Toyota Landcrusser kuacha njia na kupinduka bondeni wakati wakiwa kwenye ziara ya Makamu wa Rais,Dkt. Mohamed Bilal iliyotokea jana eneo la Nduu Mombo mpakani mwa wilaya ya Lushoto na Korogwe.
Askari wa kikosi cha kutuliza ghasia (FFU) Mkoani Tanga wakipata msaada wa kuvutwa kutoka kwenye bonde baada ya gari yao kuacha njia na kuelekea bondeni wakiwa kwenye msafara wa ziara ya makamu wa Rais Dkt. Mohamed Balil eneo la Nduu Mombo lililo mpakani mwa wilaya ya Lushoto na Korogwe jana na kusababisha vifo vya kwa askari wawili wa kikosi cha hicho.
Mmoja wa Majeruhi wa katika ajali hiyo akipata matibabu katika hospital ya Magunga wilayani Muheza.
Wananchi wa Mombo na viongozi wa Serikali wakiangalia ajali hiyo mbaya iliyotokea eneo la Nduu Mombo na kupoteza maisha kwa askari wawili na kujeruhi wanne wa kikosi cha kuzuia ghasia (FFU) Mkoa wa Tanga wakati wakitokea Lushoto kwenye ziara ya makamu wa Rais Dkt. Mohamed Bilal.

No comments: