Friday, January 13, 2012

JAMBAZI SUGU LAUWAWA ARUSHA

Na Mary Ayo-Arusha

HATIMAYE jambazi Pokeaeli Samson Kaaya au Kaunda lilokuwa likisakwa
na Jeshi la polisi mkoani hapa ambaye alifanya tukio tarehe 03
january la kumjeruhi Afisa wa polisi ASP.Faustine Mafwele pamoja na
kumuua askari EX.F.2218D/C KIJANDA kwa kumpiga risasi shingoni
ameuawa kwa kupigwa risasi na askari wa jeshi la polisi usiku wa
kuamkia leo katika kijiji cha orarashi wilayani Arumeru.

Akizungumza na waandishi wa habari, Kamanda wa polisi mkoa wa Arusha
Thobias Andengenye amesema kuwa polisi kwa kushirikiana na wananchi
waliendelea kumfuatilia jambazi huyo kwa karibu ambapo jana majira ya
saa nane usiku polisi walifika eneo la tukio na kufanikiwa kuzingira
nyumba ya ya Anna Roshirari.

Andengenye alieleza kuwa majira ya saa 06.45 asubuhi gafla jambazi
huyo ailchomoka ndani ya boma hilo na kuanza kukimbia ambapo askari
walimfukuza umbali wa kilometa mbili ambapo jambazi huyo ailimgeukia
gafla askari namba E.9912d/c WITO aliyekuwa karibu kumkamata na
kumvamia ambapo ailimjeruhi jichoni pamoja na kumuuma kidole gumba.

Kamanda aliendelea kudai kuwa askari wenzake walifika na kumpiga
risasi jambazi huyo kwa lengo la kumpunguza nguvu ndipo gafla
alianguka chini na kufariki dunia kabla ya kufikishwa hospitalini.

Hataivyo andengenye amesema kuwa jambazi Kaunda alifika kwa anna
Roshirali kwa lengo la kutibiwa kwa mganga wa kienyeji jeraha
ililokuwa amejeruhiwa mguuni siku ya tukio kwa kuhofiwa kutibiwa
hospitali kwa kuwa alikuwa ansakwa na jeshi la polisi.

Pia amesema kuwa jeshi la polisi limefanikiwa kukamata silaha
alizokuwa akitumia marehemu huyo kuwa ni pamoja na SMG No 1016188011
, risasi 20,Shortgun Moja yenye Model 88-12GA,risasi nne ambapo
zilikuwa zimehifadhiwa ndani ya mfuko wa salvet na kufichwa kwenye
kichaka.

Aidha Bw Andengenye alisema kuwa katika tukio hilo watu wanne
wanashikiliwa na jeshi la polisi ambapo watu hao ni pamoja na mke wwa
marehemu Agness Silas(40), Josephat Haule(33),Juma Salum(46},pamoja
na Dainess Masawe(19).

Vilevile jeshi la polisi linawasaka washiriki wa kaunda ambaye mmoja
wapo ni Augusti Shine au Baba Mzungu mkazi wa sakina juu.

Mwili wa marehemu umehifadhiwa katika hospitali ya mkoa ya mount meru.
Habari kwa Hisani ya Michuzi Blog

No comments: