Saturday, January 14, 2012

JUST IN ........: MBUNGE WA VITI MAALUM WA CHADEMA,MH. REJIA MTEMA AFARIKI DUNIA AJALINI LEO

Taarifa iliyoifikia Globu ya Jamii hivi punde toka mkoani Pwani,zinaeleza kuwa Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Morogoro kupitia tiketi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA),Mh. Rejia Mtema amepata ajali mbaya sana mapema leo asubuhi katika eneo la Ruvu na kufariki dunia papo hapo wakati akiwa safarini kuelekea Mkoani Morogoro.

Kwa Mujibu wa mashuhuda wa ajali hiyo walisema kuwa mbunge huyo ambaye alikuwa akiendesha mwenyewe gari lake amepinduka na gari hilo mara baada ya kumshinda wakati akijaribu kulipita gari lililokuwa mbele yake katika eneo hilo la Ruvu.

Ndani ya Gari hilo kulikuwa kuna watu wengine wanne ambao bado hawajatambulika ni kina nani na wako kwenye hospitali ya Tumbi Kibaha mkoani Pwani kwa Matibabu.


HABARI KWA HISANI YA MICHUZI BLOG

No comments: