Tuesday, January 17, 2012

MAANDALIZI YA KUAGA MWILI WA MAREHEMU MHE. REGIA ESTELATUS MTEMA, (MB), TAREHE 17 JANUARI, 2012 KATIKA VIWANJA VYA KARIMJEE NA MAZISHI IFAKARA, KILOMBERO, MOROGORO – TAREHE 18 JANUARI, 2012

Spika wa Bunge Mhe. Anne Makinda (Mb) akiongoza kikao cha kamati ya Uongozi kujadili ratiba ya maandalizi ya mazishi ya Mhe. Regia Mtema katika ofisi za Bunge jana.


TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI


YAH: MAANDALIZI YA KUAGA MWILI WA MAREHEMU
MHE. REGIA ESTELATUS MTEMA, (MB), TAREHE 17 JANUARI, 2012 KATIKA VIWANJA VYA KARIMJEE NA MAZISHI IFAKARA, KILOMBERO, MOROGORO – TAREHE 18 JANUARI, 2012
  1. UTANGULIZI
    Marehemu Mheshimiwa Regia Estelatus Mtema alifariki kwa ajali ya gari katika eneo la Ruvu, mkoani Pwani mnamo majira ya saa 5.30 asubuhi tarehe 14 Januari, 2012. Ofisi ya Bunge baada ya kuthibitisha kifo hicho kupitia Ofisi ya Kamanda wa Polisi Mkoa wa Pwani na baada ya Kuwasiliana na familia, mara moja ilituma Maafisa Waandamizi kwenda katika Hospitali ya Tumbi mkoani Pwani kuuchukua Mwili wa marehemu na kuuleta Muhimbili kuhifadhiwa ikiwa ni pamoja na kufanya maandalizi ya mazishi. Baada ya maandalizi hayo na kwa ushirikiano na familia na uongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni yafuatayo yamekubaliwa kufanyika:-
  1. MWILI KUAGWA NA FAMILIA TAREHE 16 JANUARI, 2012 KATIKA KANISA KATOLIKI SEGEREA
    Familia imeandaa Misa ya Marehemu katika Kanisa Katoliki Segerea siku ya Jumatatu tarehe 16 Januari, 2012 kuanzia saa 9 alasiri mpaka saa 11 jioni. Mwili wa Marehemu utaondoka Hospitali ya Muhimbili saa 7 mchana na baadae kurejeshwa tena kwa hifadhi baada ya Misa.
  1. MWILI KUAGWA RASMI KATIKA VIWANJA VYA KARIMJEE TAREHE 17 JANUARI, 2012
    Ofisi ya Bunge imeandaa utaratibu kwa viongozi wa kitaifa, Waheshimiwa Wabunge, Wananchi kuuaga rasmi Mwili wa Marehemu katika viwanja vya Karimjee siku ya Jumanne tarehe 17 Januari, 2012. Shughuli hiyo inatarajiwa kuanza saa 3.00 asubuhi na kuhitimishwa saa 5.30 asubuhi (Ratiba imeambatanishwa kama kiambatisho A). Kama ratiba inavyoonesha, Mwili wa Marehemu utaondoka katika viwanja vya Karimjee saa 5.30 asubuhi mara tu baada ya kuaga katika viwanja vya Karimjee kuelekea Ifakara, Kilombero mkoani Morogoro kwa mazishi.
  1. RATIBA YA MAZISHI YATAKAYOFANYIKA IFAKARA
    Ratiba ya tarehe 18 Januari, 2012 ambayo ndio siku ya Mazishi nyumbani kwa Marehemu Ifakara, Kilombero Mkoani Morogoro imepangwa kwa kuzingatia mila na desturi za familia. Ratiba hiyo ni kama ilivyo katika kiambatisho B. Kwa ratiba hiyo, shughuli zimepangwa kuanza saa 5 kamili asubuhi na kukamilika saa 10.30 alasiri.
  1. MAANDALIZI MENGINEYO
    Mpaka hivi sasa familia imearifu kuwa Msiba huo umepokelewa kwa hisia kubwa katika eneo alilozaliwa Marehemu Mheshimiwa Regia Estelatus Mtema na kwamba tujiandae kwa ushiriki kwa wakazi wa Kilombero takriban 1000. Aidha, Ofisi inaendelea na Maandalizi ikiwa imejiandaa kwa ushiriki wa viongozi wa kitaifa Mkoani Morogoro.
  1. SHUGHULI ZA K AMATI ZA BUNGE SIKU YA JUMANNE TAREHE 17 JANUARI, 2012
    Kutokana na uzito wa tukio hili, Ofisi ya Bunge inapenda kuutangazia Umma kuwa shughuli za Kamati za Bunge kwa jumanne tarehe 17 Janauari, 2012 ambazo zinafanyika katika Ofisi ya Bunge , Dar es Salaam, zitasitishwa hadi jumatano tarehe 18, Januari, 2012
    Ofisi ya Bunge inaungana na familia ya marehemu katika kipindi hiki kigumu cha majonzi. Mwenyezi Mungu ailaze roho ya marehemu Mhe. Regia Estelatus Mtema, (MB) mahali pema peponi. Amina.
    Imetolewa na,
    Idara ya Habari, Elimu kwa Umma na Uhusiano wa Kimataifa
    DAR ES SALAAM
    16 Januari, 2012
    KIAMBATANISHO A
    RATIBA YA KUAGA RASMI MWILI WA MAREHEMU SIKU YA JUMANNE
    TAREHE 17 JANUARI, 2012 KATIKA VIWANJA VYA KARIMJEE
    _________________
SN.MUDATUKIOMHUSIKA
1.02:00 - 3:00Ndugu, Jamaa na Wananchi kuwasiliItifaki
2.03:00-03:25Viongozi wa Vyama vya Siasa, Waheshimiwa Wabunge, Manaibu Waziri, Mawaziri kuwasili na kuketi katika nafasi zaoItifaki
3.03:25Kiongozi wa Upinzani Bungeni kuwasiliKatibu wa Bunge
4.03:30Mhe. Naibu Spika kuwasiliKatibu wa Bunge
5.03:35Mhe. Spika kuwasiliMhe. Naibu Spika
6.03:40Mhe. Waziri Mkuu kuwasiliMhe. Spika
7.03:50Mhe. Makamu wa Rais kuwasiliMhe. Spika/Mhe. Waziri Mkuu
8.03:50Mwili wa Marehemu kuwasili kwa gwaride maalum la Sergeant-At-ArmsKatibu wa Bunge
9.03:50 - 4:00Sala fupiKanisa Katoliki
10.04:00 - 04:10Wasifu wa MarehemuKatibu wa Bunge
11,04:10 - 04:15Salamu na Rambirambi za Mhe. SpikaMhe. Spika
12.04:15 – 04:40Salamu na Rambirambi

  • Vyama vya Siasa vyenye uwakilishi Bungeni:-CHADEMA,CCM, CUF, NCCR – Mageuzi, TLP na UDP
  • Kiongozi wa Upinzani Bungeni
  • Mwakilishi wa Serikali
MC
13.04:40 - 04:45Neno la Shukrani toka kwa familiaMwakilishi wa Familia
04:45 - 04:50Utaratibu wa safariKatibu wa Bunge
14.04:50 - 05:50Kuaga Mwili wa Marehemu kulingana na ItifakiMC
15.05:50Mwili wa Marehemu kuondoka Uwanjani pamoja na Waheshimiwa Wabunge, Wanafamilia na Maafisa wanaokwenda Ifakara, Kilombero kwa MazishiMC
16.06:00Viongozi wa Kitaifa kuondoka kulingana na ItifakiMC
    KIAMBATANISHO B
RATIBA YA MAZISHI YA MAREHEMU REGIA ESTELATUS MTEMA, MB YATAKAYOFANYIKA IFAKARA, KILOMBERO, MOROGORO TAREHE 18 JANUARI, 2012
______________________________


SN.MUDATUKIOMHUSIKA
1.04:00-05:00Wananchi, Familia na Viongozi wa Kitaifa kuwasili kulingana na Itifaki

  • Uongozi wa Wilaya na Halmashauri
  • Uongozi wa Mkoa
  • Viongozi wa Vyama vya Siasa
  • Waheshimiwa Wabunge
  • Waheshimiwa Manaibu Waziri
  • Waheshimiwa Mawaziri
  • Kiongozi wa Upinzani Bungeni
  • Mhe. Naibu Spika
  • Mhe. Spika
  • Mhe. Waziri Mkuu
  • Mhe. Rais
    Katibu wa Bunge
2.05:00 - 06:00Chakula cha MchanaWote
3.06:00 - 07:00MisaKanisa Katoliki, Kilombero
4.07:00 - 07:10Wasifu wa MarehemuOfisi ya Bunge (Mwajiri)
5.07:10 - 07:20Salaam na Rambirambi kutoka Uongozi wa Ofisi ya BungeMhe. Spika
6.07:20 - 07:30Salaam na Rambirambi kutoka kwenye Makundi mbalimbali ya Uwakilishi

  • Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA)
  • Vyama vya Siasa vyenye Uwakilishi Bungeni (CCM, CUF, NCCR-Mageuzi, TLP na UDP)
  • Mwakilishi wa Serikali
MC
7.07:30 - 08:00Msafara wa Waombolezaji kuelekea Makaburini na Mwili wa Marehemu kwa MazishiWote
8.08:00 - 08:30Ibada ya MazishiKanisa Katoliki, Kilombero
9.08:30 -08:45Kuweka Mashada ya Maua kulingana na Itifaki
10.08:45 - 08:50Shukrani kutoka kwa familiaMwakilishi wa Familia
11.08:50Viongozi Kuondoka kulingana na Itifaki

No comments: