Tuesday, January 24, 2012

MADAKTARI WATANGAZA MGOMO RASMI

Lile sakata la Madaktari na Serikali Limefikia Madaktari Kuamua Uamuzi Mgumu wa Kuamua Kugoma rasmi kuanzia Kesho tarehe 24/01/2012

Uamuzi huu metolewa leo katika mfulilizo wa Mikutano waliyoianza toka jumatano ya wiki iliyopita (18/01/2012) katika kujaribu kutafuta suluhu ya matatizo yao na ya Sekta ya Afya kwa Ujumla,Juhudi hizo hazikuzaa matunda kutoka kwa Serikali kuanzia ngazi ya Wizara ya Afya mpaka ofisi ya Waziri Mkuu ambapo kutozaa matunda.


Madaktari/watumishi wa afya hao wana madai kadhaa ikiwemo
  • Kuboresha Huduma za Afya nchini (hospitali na vitanda kwa kila mgonjwa inawezekana)
  • Maslahi Duni kwa watumishi wa sekta ya afya
  • Malipo kwa kazi za ziada kwani Madktari wanalipwa shilingi 10,000/= kwa kukesha na kufanya kazi masaa 36 tofauti na taratibu za serikali ambapo ilitakiwa walipwe shilingi 40,000(half pediem) kama taratibu za serikali zinavyoonesha lakini viongozi wa Wizara hasa Mama Blandina Nyoni wamekuwa wakikwamisha hili.
  • Haki ya kupewa nyumba au posho ya Nyumbai kama muongozo wa utumishi wa umma wa serikali ya Tanzania unavyoelekeza ule wa mwka 1994 na wa mwaka 2009..
  • Kulipwa posho ya kufanya kazi katika mazingira hatarishi(Risk allowance)
  • katiLingine ni Kuondolewa kwa Katibu mkuu wa wizara ya afya Bi.Blandina Nyoni ambaye anaonekana kuwa ni kikwazo katika juhudi za msingi katika kuboresha sekta ya afya Tanzania.
  • Bi Blandina Nyoni anatuhumiwa kutoa kauli ya kejeli kwa watumishi wa afya kuwa anamshukuru baba yake kwa kumkataza kusomea mambo ya afya kwani sekta ya ya afya haifai na ndio maana licha ya kufaulu masomo ya sayansi baba yake alimshauri asomee uhasibu.

Maamuzi hayo magumu yamefikiwa katika Mkutano wa leo uliofanyika Don Bosco Upanga DSM ikiwa ni mwendelezo wa Mikutano isiyokoma iliyoanza Toka jumatano ya Wiki iliyopita.


                                           Nawasilisha (Mdau)
Nitaendelea kutoa updates kadri niwezavyo.1 comment:

Anonymous said...

Yaani sipati picha ya Huyu bi blandina kwa kauli aliyotoa. Hao watoto wake aliowazaa aliwazalia kwa Mkunga wa jadi? Nadhani alisomea uhasibu kwa vile hana utu na Wala Hana wito. Hii ni kwa vile hakujaliwa, so to say, hekima na busara za ku-interact na watu. Na Wala sio ubaya wa field ya udaktari Otherwz angesomea vet Kama basi alikuwa bright Kama anavyojisifia Yeye Mwenyewe. Ila kufaulu kuna maana pana... Kwani Hata E ni kufaulu pass ambayo ni vigumu kukuingiza medical school but ikiwezekana kuingia uhasibu. Mh hiyo haikuwa kauli ya busara nami Nadhani Unapaswa kuomba radhi watumishi wa kada zote wa afya na vile tena madaktari hawana Imani nawe ni vizuri ukaendelea na kazi yako uliyoipenda ya uhasibu.