Monday, January 9, 2012

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali iddi:Wanatumbe Kuweni na Subira

Mhandisi wa Ujenzi wa Soko ya Samaki la Tumbe Kutoka Kampuni ya ujenzi ya ngogo iliyoko Mkoani Iringa Nd. Yussuf Bugurube akimuonyesha Balozi Seif Ramani Halisi ya Ujenzi wa Soko Hilo la Kisasa.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali iddi akikagua ujenzi wa jengo la soko la samaki la kijiji cha Tumbe Wilaya ya Micheweni baada ya kuweka jiwe la msingi ikiwa ni shamra shamra za maadhimisho ya Sherehe za Mapinduzi ya Zanzibar kutimia miaka 48.
Makamu Wa Pili Wa Rais Wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi Akitoa Mkono wa pole kuzifariji familia za wananchi wa kijiji cha Tumbe ambao walifariki baada ya kula kasa mwenye sumu hivi karibuni.Watu wanane wa familia mbili walihusika na msiba huo.
Wanafunzi Wa Ali Madrasat Hidayat Ya Kijiji Cha Tumbe Ikitowa Burdani Katika Hafla ya Uwekaji Wa Jiwe La Msingi La Soko La Samaki Ya Kijiji Cha Tumbe Mbele Ya Wageni Mbali Mbali Ambapo Mgeni Rasmi Ni Makamu Wa Pili Wa Rais Wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi.
--




Wanachi wa Kijiji cha Tumbe kiliomo ndani ya Wilaya ya Micheweni Mkoa Kaskazini Pemba wametakiwa kuwa na subra katika kipindi hichi kigumu kufuatia watu wananewa Kijiji hicho kufariki baada ya kula nyama ya Kasahapo majuzi.Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi ametoa nasaha hizo baada ya kufanya ziara fupi ya kuzifariji na kutoa mkono wa pole kwa Familia mbili zilizopatwa na masiba huo.



Balozi Seif alisema alipata habari hizo za kusikitisha ambazo familia moja pekee imepoteza watu saba kati ya wanane waliofariki kutokana na tukio hilo.

Alisema hiyo ni kudra ya Mwenyezi Muungu na wala hakuna mkono wa mtu.

“ Nyinyi mnawapenda sana jamaa zenu. Lakini tuelewe kwamba Mwenyezi Muunga anawapenda zaidi watu hao ”.Alitanabahishwa Balozi Seif.


Hivyo aliwataka wafiwa hao kundelea kuwa na moyo wa subira kwani hiyo ni njia ambayo kila kiumbe kitapita. Wakitoa shukrani zao Mmoja wa wana Familia hizo Bwana Ali Mohd Bakari wameelezea faraja yao kutokana na ujio wa Kiongozi huyo ambao unaendelea kutatinda Mapenzi kati yao na Wananchi.


Wamesema kitendo hicho kimewajengea imani na kujihisi kwamba tukio hilo sio lao pekee bali ni la Wananchi na Viongozi wote Hapa Nchini.Kasa aliyesababisha vifo hivyo alivuliwa tarehe 3 Januari na baadaye kuchinjwa kwa ajli ya kitoweyo ambapo iliwachukuwa saa 3 tuu walaji kuanza kupata athari zake.


Othman Khamis Ame

Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar

7/1/2012.



No comments: