Saturday, January 28, 2012

MBUNGE WA ZAMANI WA KALENGA MAREHEMU GALINOMA KUZIKWA KESHO

Marehemu Steven Galinoma enzi za uhai wake
Waombelezaji wakiendelea na maombolezo nyumbani kwa marehemu Galinoma kijiji cha Kalenga
Mwenyekiti wa UVCCM wilaya ya Iringa vijijini Shakra Kiwanga (kushoto) akimpa pole mjane wa marehemu Galinoma mama Ameria Galinoma ambaye ni diwani wa kata ya Kalenga (CCM) kati kati ni mtoto wa mwisho wa marehemu Galinoma
Aliyekuwa mbunge wa jimbo la Kalenga kati ya mwaka 1995-2000 na 2005-2010 Marehemu Steven Galinoma (CCM) aliyefariki dunia juzi mchana wakati akikimbizwa hospital teule ya wilaya ya Iringa (Ipamba) kuzikwa kesho mchana kitongiji cha Igawa Kalenga .

Mjane wa marehemu Ameria Galinoma ameueleza mtandao huu wa www.francisgodwin.blogspot.com kuwa ratiba ya mazishi itaanza mida ya saa 7 mchana kwa ibada itakayofanyika katika kanisa la RC Tosamaganga na baada ya hapo mwili utasafirishwa hadi makabuli ya Igawa Kalenga kwa mazishi .

Hata hivyo walisema hadi sasa bado hawajapata taarifa ya mgeni atakayeongoza mazishi hayo japo tayari viongozi mbali mbali wa chama na serikali ngazi ya wilaya hadi mkoa wamepata kufika kutoa mkono wa pole.

Mtandao huu umemtafuta mkuu wa mkoa wa Iringa Dr.Christina Ishengoma (MB) ili kujua kama ofisi yake tayari imepata taarifa ya kiongozi yeyote wa kitaifa atakayefika kushiriki mazishi hayo ,amedai bado na kuwa iwapo atapokea taarifa ataujulisha mtandao huu na kuongeza kuwa kwa upande wake atashiriki mazishi hayo .
Habari kwa Hisani ya Freancis Godwin Blog

No comments: