Wednesday, January 18, 2012

Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Injinia Stella Manyanya:Kuuza Mahindi Nje Ya Mkoa Wa Rukwa RUKSA Kwa Atakayetimiza Masharti

Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mhe. Injinia Stella Martin Manyanya (MB)
--
KIBALI CHA KUUZA MAHINDI NJE YA MKOA WA RUKWA
MKUU WA MKOA WA RUKWA ANAPENDA KUWATANGAZIA WANANCHI WOTE KUWA MKOA UMERUHUSIWA KUUZA MAHINDI NJE YA MKOA NA NJE YA NCHI.
VIBALI VYA KUUZA MAHINDI HAYO VINATOLEWA NA OFISI YA MKUU WA MKOA BAADA YA KUTIMIZA VIGEZO AU MASHARTI YAFUATAYO:-
1. MAHINDI HAYO YATAKAGULIWA NA MAAFISA KILIMO TOKA WILAYA HUSIKA NA OFISI YA MKOA ILI KUONA KAMA YANAKIDHI VIWANGO VYA KUSAFIRISHA KWENDA NJE YA NCHI NA PIA KURATIBIWA.
2. UTHIBITISHO WA KUWEKWA DAWA YA KUUA WADUDU (FUMMIGATION CERTIFICATE) NA MTAALAM ANAYETAMBULIKA NA SERIKALI.
3. BEI ELEKEZI: BEI YA KUNUNUA MAHINDI TOKA KWA WAKULIMA NI SHILINGI MIA TATU HAMSINI (350/=) KWA KILO AU ZAIDI.
4. MUOMBAJI WA KIBALI LAZIMA AWE NA LESENI YA BIASHARA. KAMA MASHARTI HAYO YOTE YATATIMIZWA KIBALI KITAPATIKANA NDANI YA WIKI MOJA.
TAFADHALI ZINGATIA TARATIBU HIZO ILI KUEPUKA USUMBUFU USIO WA LAZIMA.
TANGAZO HILI LIMETOLEWA NA
OFISI YA MKUU WA MKOA RUKWA
ENG. STELLA MARTIN MANYANYA (MB)
MKUU WA MKOA WA RUKWANo comments: