Monday, February 13, 2012

KIJANA AKUTWA AMEJINYONGA CHUMBANI KWA MAMAKE- AACHA UJUMBEkijana Raphael Steven (18) mkazi wa Mwangata katika Manispaa ya Iringa akiwa amejinyonga kwa kutumia kanga ndani ya chumba cha mama yake mzazi usiku huu(tunaomba radhi kwa picha hizi)
Umati wa wananchi wa Mwangata wakitazama mwili wa kijana huyo
Ujumbe mzito alioacha kijana huyo kabla ya kujiua wakutwa ndani ya chumba chake
Dawa ya kuua wadudu ambayo alikuwa amedai kuwa amekwenda kuipulizia ndani ya chumba cha mama yake
Kijana Raphael Steven (kushoto) enzi za uhai wake akiwa na rafiki yake
Polisi wakiondoka na mwili wa kijana huyo baada ya kuutoka katika kitanzi

NA FRANCIS GODWIN MZEE WA MATUKIO DIMA BLOG

Vilio na simanzi zimetanda katika eneo la Mwangata katika Manispaa ya Iringa kufuatia kifo cha kijana Raphael Steven (18) ambaye alikuwa akijishughulisha na kazi ya kusajili laini za kampuni ya Tigo mjini Iringa ,kufuatia uamuzi wake wa kukatisha maisha yake kwa kujinyonga kwa kutumia kipande cha kanga ya mama yake mzazi ndani ya chumba cha mama yake huyo.


Tukio hilo ambalo limeacha maswali kwa wananchi wa Mwangata huku baadhi yao wakishindwa kujizuia kumwaga machozi limetokea usiku huu majira ya saa 9 hivi baada ya mama mzazi wa kijana huyo kubaini kijana wake huyo akining'inia katika chumbani kwake baada ya kujinyonga .
Ndugu wa karibu na kijana huyo walidai kuwa majira ya saa 2 usiku alimuaga bibi yake kuwa anaingia chumbani kwa mama yake mzazi kwa ajili ya kumsaidia kupulizia dawa ya kuua mbu na kuwa mbali ya kukatazwa kuingia chumbani kwa mama yake bado alilazimisha kuingia kuifanya kazi hiyo.


Inadaiwa kuwa baada ya kuingia katika chumba hicho aliufunga mlango kwa ndani ya kuigiza kupuuliza dawa ila kutokana na masaa kuzidi kuyoyoma bila kutoka ndipo walipoamua kusukuma mlango na kumwona kijana huyo akiwa amekufa kwa kujinyonga kwa kamba hiyo ya upande wa kanga ya mamake mzazi.


Kijana huyo mbali ya kuufunga mlango pia aliiharibu taa ya ndani ya chumba hicho na kupelekea chumba chote kuwa giza na kuchukua dumu tupu na kusimamia katika paa ya nyumba hiyo na kuifunga kamba hiyo na baada ya kuingiza shingo yake katika kitanzi hicho alilisukuma dumu hilo na kuanguka chini na yeye kubaki akining'inia juu na kufa.


Mashuhuda walioteta na mtandao huu wa www.francisgodwin.blogspot.com walidai kuwa kijana huyo mchana wa leo alionekana mtaani akiwa na mawazo tele na hakuna na muda wa kuzungumza na mtu kama siku za mwanzo .


Hata hivyo mashuhuda hao walisema kuwa kwa siku ya jana kijana huyo alionekana katika ukumbi mmoja wa starehe na kuzuiwa kuingia katika ukumbi huo baada ya kukosa kadi ya mwaliko .


Habari zinadai kuwa kijana huyo alikuwa hana makuu na mtu na kuwa siku zote alikuwa ni kijana mwenye kuheshimu wakubwa na wadogo na kuwa hata kifo chake bado kinaacha maswali kwa wananchi wa eneo hilo.


Zipo habari zinazodai kuwa kijana huyo amekufa kifo kama kile cha baba yake mzazi aliyekufa kwa kujinyonga mwaka 2002 kwa wakati huo walikuwa wakiishi eneo la Isoka mjini Iringa.


Mtandao huu wa www.francisgodwin.blogspot.com umebaini kukuta ujumbe wa maandishi ambao marehemu huyo alipata kuuacha kabla ya kifo chake katika meza ya chumba chake na katika ujumbe huo amepata kuacha maneno mazito yakiwemo ya kutaka asisumbuliwe mtu yeyote kwa kifo chake na kuwa kuwaaga baadhi ya marafiki na mpenzi wake mmoja pamoja na mama yake mzazi na kudai kuwa maisha ya Dunia Jembe lenu natangulia nilikotokea.


"Asisumbuliwe mtu kwa kifo changu na na kutaja majina ya rafiki zake na mpenzi wake (ambayo yamehifadhiwa huku akimalizika na neno .Respect..Don't Cry Momy and Rukia!!...Pole mama nimeamua kumfuata baba angu!!" ulisomeka ujumbe huo ambao ameacha marehemu

No comments: