Monday, February 20, 2012

RAIS DK. JAKAYA KIKWETE AONGOZA SHEREHE ZA UZINDUZI WA MRADI WA UWEZESHAJI MIFUGO (SEED STOCK) KWA KAYA ZA WAFUGAJI WALIOPOTEZA MIFUGO

Viongozi wa kabila la Kimasai(Laigwenani) wakimpa Rais Dr.Jakaya Mrisho Kikwete zana za kijadi za uongozi mkuki na fimbo wakati wa hafla ya kukabidhi ng’ombe iliyofanyika wilayani Longido jumapili .
Mzee wa Kimasai mkazi wa Longido akimshukuru na kumuombea dua njema Rais Dr.Jakaya Mrisho Kikwete baada ya mzee huyo kukabidhiwa ng’ombe watano na mbuzi watano wilayani Longido jana.Mzee huyo ni mmoja wa wafugaji walipoteza mifugo yao yote kufuatia ukame mkali uliozikumba wilaya za Longido,Ngorongoro naMonduli.
Rais Dr.Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na baadhi ya wakazi wa wilaya Longido muda mfupi baada ya kuwasili wilayani hapo ambapo aliongoza shughuli ya kutoa msaada wa ng’ombe zaidi ya elfu ishirini na tano na mbuzi zaidi ya elfu kumi na tano kwa wakazi wa wilaya za Longido,Ngorongoro na Monduli ambao mifugo yao yote iliangamia wakati wa kiangazi kikali.
Mwanafunzi Godlisten Ole Olais anayesoma kidato cha pili katika shule ya Sekondari ya Longido akiteta jambo na Rais Dr.Jakaya Mrisho Kikwete muda mfupi baada ya Rais Kikwete kuwasili katika viwanja vya sekondari hiyo kuongoza uzinduzi wa wa mradi wa serikali wa uwezeshaji mifugo(seed stock) kwa kaya za wafugaji waliopoteza mifugo yote kutokana na ukame msimu wa 2008-2009 na 2009-2010 zilizofanyika wilayani longido jumapili.

Viongozi wa kabila la Kimasai(Laigwenani) wakimpa Rais Dr.Jakaya Mrisho Kikwete zana za kijadi za uongozi mkuki na fimbo wakati wa hafla ya kukabidhi ng’ombe iliyofanyika wilayani Longido jumapili.
(PICHA NA FREDDY MARO).

No comments: