Wednesday, February 15, 2012

WANASIASA WATAKIWA KUACHA MALUMBANO NDANI YA MANISPAA

NA Mary Ayo,Arusha

WANASIASA mbali mbali wa mkoa wa Arusha wametakiwa kuacha malumbano na kusema kuwa hawatambuani kwani hali hiyo inachangia kwa kiwango kikubwa sana kuongezeka kwa umaskini na jamii kukosa haki zake za msingi ambazo ndizo chanzo pekee cha kuwachagua Viongozi.

Hayo yameelezwa mjini hapa na mwenyekiti wa chama cha kijamii (CCK) bw James Ndarivoi wakati akiongea na waandishi wa hahabri kuhusiana na migogoro ambayo inaendelea ndani ya mji wa arusha baina ya wanasiasa.

Bw Ndarivoi alisema kuwa wapo baadhi ya watendaji wa Serikali hususani kwenye halmashauri ya Jiji ambao wananufaika na mgogoro huo baina ya wanasiasa kwa kuwa Viongozi mbalimbali ndani ya jiji la Arusha hawatembelei Manispaa ya jiji kwa ajili ya itikadi za kisiasa.

Aliongeza kuwa hali hiyo ina matatizo makubwa sana na Viongozi wanashindwa kukumbuka ahadi ambazo walizitoa kwa wananchi hali ambayo inasababisha walengwa kukosa haki zao za msingi.

‘ukiangalia utaweza kuona kitu kinachoendelea jijini hapa kwa sababu mwanasiasa anadiriki kusema kuwa hamtambui kiongozi mwingine na kwa hali hiyo hata baadhi ya watu ambao hawana maadili wanatumia nafasi hiyo kujinufaisha kwa kuwa hawana mtu wa kuwauliza”alisema Bw Ndarivoi.

Aliongeza kuwa nao viongozi wa jiji la Arusha wanatakiwa kujua na kutambua kuwa wamechaguliwa na wananchi kwa hali hiyo basi wanatakiwa kujikita zaidi kwenye maendeleo na wala sio malumbano ya kisiasahuku wakihakikisha wanatatua kero zinazaowakabili wananchi wao.

Alibainisha kuwa endapo kama wataendelea na malumbano ambayo yanazaaa kesi za mahakama kila mara ni wazi kuwa Jiji litaendelea kukabiliwa na changamoto lukuki kutokana na kukosa ushirikiano wa kijamii.

Hata hivyo aliwataka baadhi ya viongozi ambao hawashiriki vikao vya baraza kushiriki kwani kukosekana kwao katika vikao kunasababisha kutoelewa kwa mambo yanayoendelea katika sehemu zao husika za kazi.

Mbali na hilo bw Ndarivoi alisema kuwa wao kama cha kijamii wanatarajia kufanya mabadiliko makubwa sana kwa jiji la Arusha ikiwa ni pamoja na kubadilisha na kuimarisha zaidi miundombinu

Alisema kuwa wanatarajia kutumia Katiba mbalimbali za maendeleo ambapo Katiba hizo zitaweza kuleta mabadiliko mbalimbali tofauti na sasa ambapo jiji linakabiliwa na changamoto kubwa sana.

No comments: