Thursday, March 22, 2012

BOMOABOMOA KESHO ALFAJIRI GEREZANI DAR ES SALAAMMkuu wa mkoa wa Dar es salaam Mhe.Meck Sadick akiongea na waandishi wa habari jioni ya leo juu ya bomoa bomoa ya nyumba za mtaa wa Gerezani zilizokuwa zina milikiwa na shirika la Reli pamoja na mamlaka ya bandari, Zoezi hilo litafanyika kuanzia kesho saa kumi na moja alfajiri, pia amewataka wakazi wanaoishi maeneo hayo wawe wameishahama katika maeneo hayo kabla zoezi hilo kufanyika, zoezi hilo litafanywa na kampuni ya Yono action mart.ilikupisha ujenzi wa kituo kikuu cha mabasi yaendayo kasi.
Baadhi ya wawakilishi kutoka wakala wa serikali (DART)pamoja na (YONO ACTION MART)wa kwanza kushoto ni mkurugenzi mtendaji wa (DART) Bw.Cosmas Takule.wa pili katikati Mkurugenzi mtendaji wa Yono Bi Scholastica Kevela.mwisho kulia Afisa masoko Yono action mart Bw. Joseph Assey.
(PICHA NA PHILEMON SOLOMON)

No comments: